Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi ameahidi kufutwa kwa utaratibu wa kuzuia miili ya Marehemu Hospitalini kwa sababu ya deni la matibabu.
Dkt. Nchimbi amesema haya leo Septemba 25 katika mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Kilolo, Iringa kwa kusema kuwa utaratibu huo ambao umekuwapo kwa zaidi ya miongo miwili, umekuwa ukiwasababishia Wananchi maumivu makubwa.
“Rais Samia amesema huo si ubinadamu, si utu na wala si mila zetu,” amesema akimnukuu Mgombea Urais wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.