Ila mimi ningeshauri hata humu mijini wale wenyeviti wa mitaa ilibidi wawe na atlest form four, uelewa wao mdogo unaleta changamoto sana mwingine anataka rushwa hata kuiomba hawezi anaishia kuongea utumbo tu!
Hata vijijini watu wapo was form 4. Nahii italeta tija watu au watoto watasoma kwa bidii wawapo mashuleni wakijua bila elimu flani siwezi kuwa hata mwenyekiti wa mtaa/kijiji. Binafsi huwa nashangaa sana kuona zikitoka nafasi za madeva au wafagia ofsi wanatangaza awe walau na elimu ya kidato cha nne ikija kwenye nafasi za ubunge na udiwani utasikia ilimradi ajue kuandika na kusoma ndo kigezo kikubwa. Halafu hawa watu ndo wanaoenda kupanga mipango ya nchi nzima hadi kwenye vyuo vikuu vinavyo endeshwa na maprofesa.