Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Machi 27-29, 2023 alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo alichangia kiasi cha TZS 9,900,000/= kwaajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Maendeleo kwa Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa Ujumla.
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amemshukuru Rais Samia kwa kutoa Milioni 371,454,739.95/= kwaajili ya Ujenzi wa Mradi mkubwa wa Maji wa Mabawe kwa Wananchi wa Murugina na Mukaliza ambapo mpaka Mwezi Machi 2023 vituo 16 vinatoa Maji.
Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amesema wananchi wa Kata ya Mabawe waliishi bila uhakika wa Maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 42.
Aidha, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameendelea amemshukuru Rais Samia kwa kukubali kuidhinisha zaidi ya TZS Bilioni 153.56 kwaajili ya Ujenzi wa barabara ya Lusahunga - Rusumo kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 92.
#AliahidiAmetekeleza
#MamaKazini
#MiakaMiwiliYaMama