Ndaisaba Ruhoro anauliza; Ni Upi mkakati wa Serikali wa kuwezesha Vituo vya Forodha vya Murusagamba na Kabanga, kufanya kazi saa 24

Ndaisaba Ruhoro anauliza; Ni Upi mkakati wa Serikali wa kuwezesha Vituo vya Forodha vya Murusagamba na Kabanga, kufanya kazi saa 24

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

sddefaultwedfsaqw.jpg

Serikali imesema kuwa inafanya jitihada ili Kituo cha Forodha cha Pamoja (OSBP) Kabanga, kinachotoa huduma kati ya Tanzania na Burundi, kiweze kutoa huduma saa 24 ili kuongeza ufanisi.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoho, aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuwezesha Vituo vya Forodha vya Murusagamba na Kabanga, kufanya kazi saa 24.

Mhe. Chande alisema kuwa Kituo cha Forodha cha Kabanga ni Kituo cha Pamoja (OSBP) cha kutoa huduma za forodha kati ya Tanzania na Burundi ambacho kina miundombinu wezeshi kama vile taa za ulinzi, vyombo vya ulinzi na usalama, na maeneo ya kukagulia bidhaa, wasafiri na wafanyakazi, hivyo kuwa na uwezo wa kufanya kazi saa 24 kwa upande wa Tanzania.

“Ili Kituo hicho kiweze kutoa huduma saa 24, upande wa Kobero nchini Burundi unapaswa pia kuwa tayari kutoa huduma hizo saa 24”, alieleza Mhe. Chande.

Alisema kuwa kwa sasa Kituo cha OSBP Kobero kwa upande wa Burundi kinatoa huduma kwa saa 12 tu, hivyo jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuwezesha mazingira ya Kituo cha OSBP Kobero kufanya kazi saa 24, hususan ulinzi na usalama.

Akieleza kuhusu Kituo cha Murusagamba, Mhe. Chande alisema kuwa Kituo hicho ni kidogo cha forodha kinachofanya kazi ya uzuiaji (Preventive office), ambapo hufanya kazi ya kuzuia magendo kwenye maeneo ambayo mwenendo wa bidhaa na watu ni mdogo.

Naibu Waziri Mhe. Chande alisema kuwa, kutokana na udogo wa mwenendo wa bidhaa na watu katika Kituo cha Murusagamba uwezekano wa kituo hiki kufanya kazi saa 24 kwa sasa haupo.

Akijibu maswali ya nyongeza kuhusu ufungaji wa kifaa cha ukaguzi (Scaner) eneo la Mtukula lililopo mpaka wa Tanzania na Uganda na Kituo cha Horohoro Tanga kati ya Tanzania na Kenya, Mhe. Chande alisema kwa upande wa Mtukula, tayari Mkandarasi yupo eneo la mradi kwa ajili ya kufunga kifaa hicho na upande wa Horohoro, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaangalia utekelezaji wake.
 

Attachments

  • 3 (11)vcfrty.JPG
    3 (11)vcfrty.JPG
    71.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom