Ndani ya miaka 4 ya Rais Samia, TRA yakusanya TZS 121 Trilioni

Kwa takwimu hizo tunastaili kujipongeza lkn na nilazima pia tuwe na masikitiko. Kwa nini nasema hivyo bado taratibu za ukusanyaji kodi hazijawa madhubuti. Watu wanakusanya kodi kwa mazoea. Na kama kuna eneo linaongoza kwa ukwepaji kodi na Kariakoo imo hata kama watanuna ukweli ndio huo. Pale Kariakoo ni mabilioni ya pesa yanapotea kwa siku. Maduka ya simu ndio usiseme kabisa.
 
Unaandika Kwa kutumia hisia au? Madeni hayaji ghafla hivyo yanalipwa mdogo mdogo kadiri ya makusanyo.

Mwisho mikopo ipo kufidia gap ya Bajeti (deficit)
 
Hesabu zikae sawa ni 121-91=30T clear gap ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ
 

Mambo 20 Chini ya Rais Samia​


  1. Diplomasia ya Uchumi โ€“ Amefungua Tanzania kwa dunia, kurejesha mahusiano mazuri ya kimataifa na kuvutia wawekezaji.
  2. Miradi ya Maji โ€“ Utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji vijijini na mijini, kuhakikisha wananchi wanapata huduma safi na salama.
  3. Sekta ya Afya โ€“ Ujenzi na ukarabati wa hospitali, vituo vya afya na zahanati nchi nzima; kuongeza vifaa tiba na dawa.
  4. Sekta ya Elimu โ€“ Kuondoa ada kwa shule za sekondari hadi kidato cha sita na ujenzi wa shule mpya pamoja na mabweni.
  5. Barabara na Miundombinu โ€“ Ujenzi na ukarabati wa barabara kuu na za vijijini, madaraja na barabara za mchepuo mijini.
  6. Mradi wa Umeme Vijijini โ€“ Upanuzi mkubwa wa REA unaowafikia wananchi wengi zaidi vijijini.
  7. Umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) โ€“ Kuendeleza mradi wa umeme wa megawati 2,115 kwa maendeleo ya taifa.
  8. Uboreshaji wa Shirika la Ndege (ATCL) โ€“ Kununua ndege mpya na kuongeza safari za kimataifa.
  9. Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) โ€“ Kuendeleza mradi wa reli ya umeme kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
  10. Uwekezaji katika Bandari โ€“ Kuboresha bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ili kuongeza biashara na mapato.
  11. Ajira kwa Vijana โ€“ Kupitia miradi ya kilimo (Building a Better Tomorrow โ€“ BBT) na sekta nyingine.
  12. Kilimo na Chakula โ€“ Kutoa ruzuku ya mbolea na pembejeo, kuanzisha Programu ya Kilimo cha Kibiashara.
  13. Mikopo ya Halmashauri 10% โ€“ Kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu.
  14. Mapambano dhidi ya Ufisadi na Rushwa โ€“ Kuimarisha uwajibikaji na uwazi katika taasisi za umma.
  15. Sekta ya Madini โ€“ Kuboresha mikataba ya madini ili Tanzania inufaike zaidi.
  16. Michezo na Sanaa โ€“ Kuwezesha vijana kushiriki kimataifa na kuanzisha mfuko wa kuendeleza sanaa.
  17. Afya ya Mama na Mtoto โ€“ Kujenga vituo vya kisasa vya huduma ya dharura na kuongeza watoa huduma.
  18. Mfumo wa Kidigitali Serikalini โ€“ Kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma.
  19. Utalii na Hifadhi za Taifa โ€“ Kutangaza Tanzania kimataifa kupitia filamu, promosheni na uwekezaji.
  20. Amani na Umoja wa Kitaifa โ€“ Kuimarisha mshikamano wa kijamii, kisiasa na kuendeleza majukwaa ya mazungumzo ya kitaifa.
 

View: https://www.instagram.com/p/DWlTf1njJD-/?igsh=MWFybDg1YzN2M3B2Ng==
 
Kama ni kweli mbona hayo matrilioni haya akisi kasi ya maendeleo ya Nchi?. Zaidi deni la taifa linakua kwa kasi.

Kwanini miradi mingi ya maendeleo imesimama?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ