NDC, NEEC kuanza kuwezesha wananchi

NDC, NEEC kuanza kuwezesha wananchi

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
666
Reaction score
426
SHIRIKA la Maendeleo la Taifa (NDC) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), yametangaza kuunganisha nguvu katika kukuwezesha wananchi, kupitia miradi inayoendeshwa na NDC.


Hatua hiyo inayoashiria Serikali kukunjua makucha dhidi ya migogoro baina ya wananchi na wawekezaji.


Katibu Mtendaji wa NEEC, Anaclet Kashuliza na Mkurugenzi wa Viwanda vya Kuongeza Thamani wa NDC, Shanel Mvungi walisema hatua hizo ni za awali kuwezesha wananchi.
“Tumeanza hatua za awali za uwezeshaji wananchi kwenye maeneo jirani na mradi wa uchimbaji Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma Liganga, wilayani Ludewa, tunaamini uwezo wao wa uchumi utakuzwa,” alisema Kashuliza.


Alisema utafiti wa awali umeonyesha kuwa yapo mahitaji makubwa ya bidhaa mbalimbali, ambazo wananchi walio pembezoni mwa eneo la mradi wanaweza kuanzisha.


Aliendelea kuwa wanaweza kuzalisha na kuuza na kunufaika wa ajira za moja kwa moja na kwamba, ajira hizo siyo chini ya 5,000.
Bidhaa hizo zilitajwa kuwa ni kuku, nyanya, vitunguu, matunda mbalimbali na mboga za majani.


Kashuliza alisema watendaji wa NEEC wamefanya utafiti wa awali na kubaini jinsi wananchi wanavyoweza kunufaika.Alisema wanajiandaa kutekeleza uondoaji vikwazo vilivyobainishwa ili wananchi hao. Akizungumza kabla ya kukabidhiana mikataba hiyo, Mvungi alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakinufaika na miradi inayowekezwa maeneo yao.


“NEEC wameanzia kwenye mradi wetu wa Mchuchuma na Liganga, wataendelea na mingine tutakayoanzisha, hali itakayotofautisha miradi yetu na inayoendeshwa na wawekezaji wengine,” alisema Mvungu.


Mvungi alisema mpango huo utalenga zaidi kuwaelimisha wananchi wa maeneo jirani na miradi, kuona na kutumia fursa zilizopo, ikiwamo kuwasaidia kukuza uwezo wa kubuni na kutekeleza shughuli za uzalishaji.
 
hawamu ya kwanza ya usaidizi inaanzia kwenye makaa ya mawe halafu wanasema potential hipo kwenye miradi ambayo inaweza buniwa na watu na kuongeza ajira zaidi, sasa kwanini wasiende kuwasaidia hao wenye huwezo mkubwa wa kuleta ajira kwanza na mbona hawaelezii watawasaidia vipi?

Maana sote tunajua Tz ina maliasili lakini mbinu za kufanya zionekana zinamanufaa kwa taifa so far ni kama zero, watu hawa kweli ndio watakao weza kuja na mbinu za kuwasaidia wafugaji wa kuku bila ya kutangaza namna ya huo usaidizi utavyokuwa, hivi watu hawachoki hadithi.
 
Hizi taasisi za Serikali sitakaa ni ziamini katika kuwasaidia Watanzania, wako kimasilahi yao sana, wote wasanii na hajajitoa kwa moyo wote kuwasaidia Watanzania, Kuna Taasisi kibao za Serikali ambazo zipo kwa ajili ya kuwasaidia wajasirimali lakini hakuna kitu ni usanii mtupu na kikubwa wanaangalia jinsi ya kuunemeka kupitia hizo prodram.
 
Back
Top Bottom