Ndege Mpya ya Mizigo Iyafikie Masoko ya Nje

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Kesho Tanzania itapokea ndege ya mizigo. Hatua hii ichukuliwe kwa uzito wa pekee na wafanyabiashara wakubwa na wadogo. Ndege hiyo kubwa ya mizigo aina ya Boeing 767-300F itakuwa na uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo na kusafiri katika nchi za Ulaya, Asia na kwingineko ambako soko litapatikana.

Ujio wa ndege hiyo ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara nchini kupanua masoko yao kwani ina uwezo wa kusafiri katika nchi nyingi kwa muda mfupi hali itakayosaidia bidhaa kufika ikiwa bado katika ubora wake.

Naamini wafanyabishara wa mbogamboga, matunda, samaki na nyama wataichangamkia zaidi fursa hiyo.
Nasema hivyo kwa sababu naamini kabla ya ujio wa ndege hiyo, walikuwa wanapata tabu ya kusafirisha bidhaa hizo kwenda kwenye masoko ya nje kutokana na gharama kubwa ya kutumia ndege za mizigo za mashirika ya ndege ya nchi jirani.

Kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetatua tatizo hilo, nivyema sasa kwa wafanyabiashara wakatumia ndege hiyo ipasavyo kwa kuhakikisha wanayafikia masoko
yote muhimu yanayohitaji bidhaa za Tanzania. Uzuri wa ndege hiyo, kama ilivyoelezewa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, ni kwamba inaweza kukodishwa pia kwa wafanyabiashara wanaohitaji kusafirishia bidhaa zao.

Hilo si jambo dogo. Jambo muhimu la kusisitiza ni kwamba, hii ni ndege imenunuliwa kwa kodi za wananchi, hivyo ipewe nafasi ya kutosha katika kusafirisha mizigo ya ndani na nje ya nchi ili lengo lililokusudiwa litimie. Ikiwa Watanzania wataitumia vyema na kuleta matokeo chanya, naamini serikali ya Rais Samia inaweza kufikiria kuongeza ndege nyingine kama hiyo au kubwa zaidi kwa ajili ya kusaidia kukuza biashara.

Kwa kuwa bado kuna uhitaji wa vyumba vya baridi katika viwanja vya ndege, ni vyema Watanzania wenye uwezo wachangamkie fursa hiyo kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu hiyo.

Ni matumaini yangu kwamba jitihada hizi za serikali zitaungwa mkono kuhakikisha wafanyabiashara wa Tanzania wanapata mazingira bora ya kufanya shughuli zao ndani na nje ya nchi na kutanua wigo wa biashara katika kuyafikia masoko makubwa ya nje.​
 
Baada ya miezi 6 itabaki ajili ya matengenezo na ndiyo mwisho wake, ziko wapi zile ndege ambazo zilikuwa zinapokelewa kwa mbwembwe usiku usiku? nusu ya zile ndege zimebaki muda mrefu sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…