Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 236
matatizo ktk biashara ya ndege ni kitu cha kawaida,kuna hali ya hewa,na mengineyo meengi,sasa kwa precision kulaza mara 3,mwezi uliopita sio kweli,pili ililaza mara moja,na ni abiria wa mombasa,sababu ilikua hali ya hewa mbaya,na wasingeweza kurisk maisha ya abiria,
hivi mchina na mhindi yupi afadhari jamani naombeni msaada hapo.....yupi ni bora tumkumbatie?
mchina ana kwake mhindi hana kwake bora mchina una uhakika ya kupambana nae
Hapana,mkubwa,precision hua hailazi,abiria uwanjani,hua inalaza abiria hotel zenye hadhi flani,ili mteja awe confortable,kwa mfano huko mwanza,huwa wanalala mwanza hotel au,lakairo,kwa dar wanalala markham au holiday inn,siku hizi inaitwa sunrise in,au peackock,kwa hiyo kaka,sie tunawajali abiria wetu,
hivi mchina na mhindi yupi afadhari jamani naombeni msaada hapo.....yupi ni bora tumkumbatie?
Lione,
Huu ndiyo umuhimu wa kujiunga JF maana hali ya hewa ikichafuka unatetea kampuni yako. Bravo😉
Quote:
Originally Posted by Mama Mia
Mmmh uwanja wenu wa nyerere mshampa mchina
kampuni ya ndege ya taifa mshampa mchina
bado ikulu
Sijakusoma vyema hapo mama 100!
__________________
yaani uwanja wa nyerere uko katika nyakati za mwisho kukabidhiana na wachina kampuni ya sonagol ambayo ndiyo hiyo muda si mrefu wanakabidhiwa kampuni ya ndege ya taifa yaani atcl!!na kukabidhiwa asilimia 49 kazi kweli kweli!!mnakumbuka nilisema hawa wamekuja kwenye madini habari za uhakika ni kwwamba wamepelekwa pia kwenye madini kule mwanza na shinyanga na baadhi wameomba kwenda na mbuguni arusha kucheck!!maslahi jamanitanzania imekuwa kweli kichwa cha mwenawazimu
Hivi Mchina na Mhindi yupi afadhari jamani naombeni msaada hapo.....yupi ni bora tumkumbatie?
Fidel,
In terms of technology, ningekushauri kwa asilimia 99 utumie teknolojia za wahindi kuliko za wachina, kwa sababu tu kwamba teknolojia za wahindi zinadumu sana kuiko za wachina, "KWA SOKO LA AFRIKA". Mfano ukianzia katika teknolojia ya magari, sina shaka kabisa kwamba "Toyota DCM na Tata" za wahindi ni bora mara mia kuliko "Faw, Jiefang, Dong Feng, Aeolus, Yue Jin nk" za wachina.
Hata kwa sie mainjinia, power generators za India kama vile kutoka kampuni za Tata ama Kirloskar za ukubwa ule ule zinadumu zaidi kuliko za Jian Dong za kichina, hii ni kutokana na uzoefu wangu katika kazi zangu.
Need I say more?
Idimi,
Wanasema kuwa Wachina ni pesa yako. Ukitaka gari la dola 5,000 utapata. Ukitaka gari la dola 20,000 utapata nk. Sasa kwa UROHO wa 10% kwa viongozi wetu basi wanaenda kuzoa wakifikiri wamepata kumbe wamepatikana. Kumbuka wamewalazimisha AIR BUS kwa mara ya kwanza waanze kuzalisha ndege zao China. hii ilikuwa na donge nono la kununua kutoka Airbus ndege kama sikosei zaidi ya 100 huku wakinunua Boeng kama sabini na kitu. China kuna viwanda kibao na hiyo imewafungua sana macho. Kuna jamaa yangu humu ndani anafanya kazi HUAWEI, na siku moja nilimcheka kuwa nimeona ROUTER yao moja dukani. Akasema kuwa wao ni wakali sana kwa vifaa hivyo. Na ni kweli maana hata Tanzania hii kampuni inaingia.
Kwenye magari pia wanakuja juu sana. Tayari wameshaanza kutengeneza HYBRID cars. Pia wanauza hata EU. Nilikuwa nasoma ugomvi wa gari lao moja na BMW. Jamaa wamekopi X5, Toyota na sijui gari gani kwa muundo. Kumbuka EU hadi waruhusu gari hasa Wajeruman basi lazima likidhi jizo ISO zao. Tanzania sisi twataka bei poa, basi na wao wanapoa na kulipua kazi na materials. Tanzania itategemea sisi wenyewe na ulafi wetu. Zikianza kudondoka watu watagoma kupanda.
Ukweli twapenda sio 10% ni 100%Idimi,

Kaka,sio tu kutetea,ni ukweli ulio dhahiri kabisaa,ni kama vile tofauti ya togwa na bia,you can test it and feel it,atcl wanamambo mengi sana ya kufanya kufikia kiwango cha precision air,na ukweli kwamba precision sasa ndio leading airline hapa nchini uko wazi,na hata yule aliesema ndege imekaa pale airport,namshangaa,maana ndege airport ndo nyumbani kwake,sio kwenye soccer field,however,tuiunge mkono precision jamani.its our national pride