Ndege ya Delta Yapata Ajali Toronto, Watu 15 Wajeruhiwa

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Watu 15 akiwemo Mtoto, wamejeruhiwa huku baadhi yao wakiwaishwa Hospitali kutokana na majeraha waliyoyapata baada ya Ndege ya Delta ya Nchini Marekani kupata ajali leo kwa kubinuka juu chini kwenye njia ya kurukia Ndege baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Toronto Nchini Canada.

Hata hivyo hakuna kifo chochote kilichosababishwa na ajali hiyo ambayo imehusisha Ndege ya Delta namba 4819 iliyotokea Minneapolis Marekani kwenda Toronto, Canada ikiwa na Abiria 80 ambao wote wameondolewa kwenye Ndege hiyo tayari.

Soma Pia: Marekani: Ndege iliobeba raia 64 imegongana hewani na helicopter ya kijeshi na kusababisha vifo kadhaa

Kubinuka kwa Ndege hii kumetokea wakati upepo mkali
20250217_234903.jpg
 
Sipati picha kama ingekuwa imetokea China,Russia,Korea kaskazini,Iran au Tanzania.

Hizo dhihaka zingekuwa hazina idadi.
Huwezi kuwaona wa State Toka Inyonga na Mngeta wakijisemea Mbovu.
 
Watu 15 akiwemo Mtoto, wamejeruhiwa huku baadhi yao wakiwaishwa Hospitali kutokana na majeraha waliyoyapata baada ya Ndege ya Delta ya Nchini Marekani kupata ajali leo kwa kubinuka juu chini kwenye njia ya kurukia Ndege baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Toronto Nchini Canada.

Hata hivyo hakuna kifo chochote kilichosababishwa na ajali hiyo ambayo imehusisha Ndege ya Delta namba 4819 iliyotokea Minneapolis Marekani kwenda Toronto, Canada ikiwa na Abiria 80 ambao wote wameondolewa kwenye Ndege hiyo tayari.

Soma Pia: Marekani: Ndege iliobeba raia 64 imegongana hewani na helicopter ya kijeshi na kusababisha vifo kadhaa

Kubinuka kwa Ndege hii kumetokea wakati upepo mkali
View attachment 3239917
Sipati picha kama ingekuwa imetokea China,Russia,Korea kaskazini,Iran au Tanzania.

Hizo dhihaka zingekuwa hazina idadi.
Ukweli ni kwamba ajali hii ingetokea kwenye nchi Kama hii ya kwetu, basi Abiria wote kabisa waliopo kwenye hiyo ndege mpaka sasa wangekuwa tayari tusingeweza tena kuwa nao tena kwenye dunia hii. Wangekuwa tayari wameshatangulia mbele za haki.
Huu ndio Ukweli, whether we like it or not.
 
Vipi na moto waliuzima kwa muda gani.
 
Udumavu wa akili ni tatizo kubwa sana Africa.

Kuna watu wanaona America na Europe hawana mapungufu kabsa wako perfect.
Unajihisi una akili yenye afya kinoma kwa hivyo viji-coment vyako! Pole.
 
Mbona tangia Trump aingie madarakani haya matukio ya ndege yamekuwa yanajirudia hapo Marekani ,au nihujuma wanamfanyia jamaa kuchafua utawala wake.
 
Majnga majanga ni ishara za laana huko. Dah.

Mungu endelea kuibariki Africa.
 
Mbona tangia Trump aingie madarakani haya matukio ya ndege yamekuwa yanajirudia hapo Marekani ,au nihujuma wanamfanyia jamaa kuchafua utawala wake.
Kwa jicho jingine, inaonekana kama ni laana tu.
 
Rubani alilazimisha kutua hali ya hewa ikiwa mbaya sana. Japopia amejitahidi kupunguza ukubwa wa ajali maana kwa hali hiyo ya hewa na utulivu wa ndege wakati inatua alijitahidi.

Video nimekutana nayo insta kuanzia ndege inatua mpaka moto unazuka. Nikaiacha sikuzingatia sana
 
Ukweli ni kwamba ajali hii ingetokea kwenye nchi Kama hii ya kwetu, basi Abiria wote kabisa waliopo kwenye hiyo ndege mpaka sasa wangekuwa tayari tusingeweza tena kuwa nao tena kwenye dunia hii. Wangekuwa tayari wameshatangulia mbele za haki.
Huu ndio Ukweli, whether we like it or not.
Ndege yenyewe wewe hujawahi panda maisha yako yote lakini unavyojifanya mchambuzi utafikiri ulishawahi kuwa rubani wakati wewe ni mwendesha bodaboda unaishi uswahilini
 
Daah hao raia wana bahati ya mtende. Kawaida ndege ikianguka kifuatacho tunatandika turubai.

NB: Kati ya december 2024 mpaka sasa ajali za ndege zilizoripotiwa dunia nzima ni 87. Source NTSB
 
Back
Top Bottom