Ndege ya kivita ya Marekani yadunguliwa kwenye Bahari Nyekundu

Ndege ya kivita ya Marekani yadunguliwa kwenye Bahari Nyekundu

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Ndege ya kivita ya Marekani imedunguliwa katika Bahari Nyekundu kwenye tukio linaloonekana kuwa "ufyatuaji wa silaha uliotokea upande wao", jeshi la Marekani limesema.

Wafanyakazi wote wa Jeshi la Wanamaji la Marekani F/A-18 Hornet walitolewa nje wakiwa salama, huku mmoja akiuguza majeraha madogo, kulingana na Kamandi Kuu.

Tukio hilo limewadia baada ya Marekani kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya eneo la kuhifadhia makombora katika mji mkuu wa Yemen Sanaa unaoendeshwa na wanamgambo wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.
Kamandi Kuu ya Marekani iliongeza pia ilishambulia ndege nyingi zisizo na rubani za Houthi na kombora la kujilinda dhidi ya meli kwenye Bahari Nyekundu.
 
Katika medani za kivita hilo ni tukio la kawaida mno - actually ni very common. Ni human errors inaitwa. God bless them. Amen.
 
Hiyo ndege imedunguliwa na Houthi ila Marekani wanaona aibu kusema ukweli ndiyo maana wanasema ni friendly fire.
 
Back
Top Bottom