Ndege ya kivita yaangusha mabomu kwenye makazi ya watu

Ndege ya kivita yaangusha mabomu kwenye makazi ya watu

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Watu saba wamejeruhiwa nchini Korea Kusini, wanne kati yao vibaya, baada ya ndege ya kivita kudondosha mabomu manane kwa bahati mbaya katika eneo la makazi ya raia wakati wa mazoezi ya kijeshi.

Tukio hilo lililohusisha ndege ya Jeshi la Anga ya KF-16 lilitokea katika jiji la Pocheon, karibu na mpaka na Korea Kaskazini.

Ni bomu moja pekee ndilo linaloaminika kulipuka.

Kikosi cha kutegua mabomu kinafanya kazi ya kuondoa kwa usalama mabomu mengine saba ambayo hayajalipuka.
Serikali ya Pocheon imeiambia BBC wakazi wanaoishi karibu na eneo hilo wamehamishwa.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya ndani, watu wawili walipata majeraha ya shingo na mabega.

Jeshi la anga la Korea Kusini limesema linachunguza tukio hilo na kuomba radhi kwa uharibifu huo na kuongeza kuwa itatoa fidia kwa walioathirika.

Jengo moja la kanisa na nyumba pia ziliharibiwa kutokana na tukio hilo. Picha zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari vya ndani zinaonyesha dirisha lililovunjika la jengo na paa la kanisa lililoharibika.

Wizara ya ulinzi imesema mafunzo hayo ya Alhamisi yalihusisha mazoezi ya pamoja na vikosi vya Marekani.
 
ulikotoa hii taarifa na wao hawajaweka picha?
 
Kwa nini unatoa habari nusu nusu?

Sema ndege ya jeshi la Marekani iliyokuwa inafanya mazoezi ya jinsi ya kushambulia North Korea imewalipua raia wa South Korea

Hapo South Korea wanaumia sana ni vile tu bwana mkubwa wake itabidi akaushe

Kuwa kibaraka wa Marekani ni uwendawazimu sana
 
Back
Top Bottom