KWELI Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

KWELI Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
1658997377303.png
 
Tunachokijua
Julai 27, 2022 kupitia Mtadao wa X (Zamani Twitter), habari za ndege ya Precision Air iliyokuwa inatoka Mwanza kwenda Dar kuzima injini ikiwa angani na kulazimika kutua Kilimanjaro kwa dharura zilianza kusambaa.

Mathalani, Mtumiaji mmoja wa Mtandao huo anayeitwa Simon Mkina alisema;

"Precision Air flying from Mwanza to Dar has lost an engine. I am onboard. Our captain has said we are landing at KIA for this emergency. He said we dont have to worry about. Flight No. PW 467. YOUR PRAYERS"

Aliendelea kusema kuwa ndege hiyo yenye namba PW 467 imetua KIA salama. Ndege nyingine PW 712 Iliyotokea Nairobi ndio iliwachukua wasafiri kuelekea Dar ambapo walipitia Zanzibar.

Hofu ilianza kutokea baada ya abiria mmoja, kijana wa kizungu, kuanza kupiga kelele, akiwaeleza wenzake waliokuwa wameketi jirani, kwamba injini imezima.

Baadaye abiria wengine waliingiwa hofu, huku baadhi wakisali, wakilia na wengine kuonekana wamejiinamia, huku wamefunika nyuso zao.

Baada ya abiria kuonekana 'wakipaniki' ndipo rubani wa ndege hiyo alitangaza kuwepo kwa hitilafu hiyo huku akieleza kwamba hali siyo ya kutisha sana.

"Abiria wetu wapenzi, ndege yetu imepata tatizo la kiufundi, injini moja imezima, lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani, tunapanga kutua katika kiwanja jirani na hapa tulipo," alisema rubani huyo.

Hata hivyo, tulizo la mwana anga huyo halikuleta afueni ya wasiwasi kwa abiria wengi, waliendelea na hofu yao, huku wengine waliokuwa hawajatambua kinachoendelea wakiungana na wengine kusononeka.

Rubani alirejea tena kwa tangazo; "Abiria wetu wapendwa, tunasikitika kwa kilichotokea, nawaomba kuwa watulivu wakati sasa tunajiandaa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Tutatua ndani ya dakika 20."

Baada ya muda huo, ndege hiyo ilitua salama katika uwanja huo na abiria walishangilia. Wengine walipiga kofi, wengine wakipiga kelele za shangwe na wengine wakimshukuru Mungu.
Back
Top Bottom