Ndege ya Shirika la ndege ATCL yatua Msalato Kwa majaribio

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kwa mara ya kwanza, ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya majaribio ya awali kabla ya kiwanja hicho kuanza rasmi kuhudumia Watanzania.

Akizungumza baada ya kuipokea ndege hiyo, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema kuwa hadi sasa ujenzi wa kiwanja hicho umefikia zaidi ya asilimia 80, huku njia za ndege zikiwa tayari zimekamilika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema kiwanja hicho kitaendelea kuutangaza Mkoa wa Dodoma na kuchochea kasi ya maendeleo. Amewahamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kesho kushuhudia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye atatembelea mradi huo wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato pamoja na barabara ya mzunguko (Ring Road) ya Jiji la Dodoma.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…