Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Mama Maria Nyerere, wameshiriki Misa Takatifu ya Kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika leo Oktoba 14, 2026, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Epifania, Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Katika ibada hiyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan huku Misa hiyo ikiongozwa na Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Damiani Kyaruzi.
Makamu wa Rais Mh. DEOGRATIUS NDEJEMBI akiwa anaagana na Waziri Mkuu, Dkt MWIGULU NCHEMBA katika Uwanja wa CCM NELSON MANDELA uliopo katika Manispaa ya Sumbawanga leo Oktoba 14, 2026.