Ndesamburo aja na hili tena


Kunya anye kuku tu, akinya bata kaharisha!!!
 
SYLL unamuuliza mzee wa Kibara kwa nini ? Unataka kujua yupo wapi ukiwa na maana ipi ? Mimi si msemaji wake ila nimeshangaa hoja hii na swali lako kwa mwana JF huyu .
 
Imekaa vema; mtu wa mada aliwachanganya; lakini ukweli ni kuwa Ndesa (kama wabunge wenzie wanavyomuita) si mtu wa makuu, lengo ni kuona maisha ya watu yanakuwa bora; na kila anachoahidi hutimiza(kaulize Moshi Mjini); wanaobisha ni wale wanaoombea adui njaa. But kuna watu ambao hakika bado naamini hawajatoka ktk mstari wa maadili, na daima wanatetea haki. Makani,Mtei, Ndessa, Lipumba, Mbowe, Mwakyembe,Zitto, Slaa (champion), Hamad, Kihwele Lucy, etc. Tuwaombeeeeee
 


Heshima Mbele mkuu.
Hii Ambulance wale wapokeaji walikuwa wanakataa kupokea, kisa? Imetoka kwa wapinzani. Mhe Ndesamburo alishwahi kulilalamikia hili suala mara kadhaa kwa Mkapa, kwamba gari alilolitoa kusaidia jamii linakataliwa na sirikali.
Sijajua hili sakata limeishia wapi mpaka leo!
 

Comrade,
Hujamtendea haki Syllogist.
Yeye kama walivyo wana JF wengine ana haki ya kutoa mawazo yake hapa jamvini, yawe ni ya kupinga ama ya kuendeleza mjadala. Hatuwezi kukubaliana kwa kila jambo hapa JF! Hili halipo!
Jamaa ana haki ya kusikilizwa hata kama atakuwa kinyume na tulio wengi!

Nawasilisha.
 

Huyu mzee hakuanza leo. Alivyopata ubunge mara ya kwanza alienda kwenye hospitali ya mkoa akabadilisha kuanzia vitanda, shuka, magodoro pamoja na ukarabati mwingine na kuwapa ambulance 2. Hivyo wapiga kura wake wanamwelewa vizuri tu.
 
Huyu mzee hakuanza leo. Alivyopata ubunge mara ya kwanza alienda kwenye hospitali ya mkoa akabadilisha kuanzia vitanda, shuka, magodoro pamoja na ukarabati mwingine na kuwapa ambulance 2. Hivyo wapiga kura wake wanamwelewa vizuri tu.

Sasa ni kitu gani kinatufanya Wadanganyika tusiwachague watu kama Mheshimiwa Ndesamburo amabao wanatoa pesa zao mfukoni ka kusaidia jamii? Natumai tungekuwa mbali sana kama tungekuwa na wabunge wenye moyo namna hii.
Katika kumbukumbu zangu, nadhani kwa sisiemu kulikuwa marehemu Abbas Gulamali (RIP) ambaye alikuwa na roho ya namna hii! Alikuwa akikodi matrekta kutoka maeneo mbali na kwenda kusaidia kulima mashamba ya wananchi
Kama kuna wengine kutoka sisiemu tuambiane!
 
SYLL unamuuliza mzee wa Kibara kwa nini ? Unataka kujua yupo wapi ukiwa na maana ipi ? Mimi si msemaji wake ila nimeshangaa hoja hii na swali lako kwa mwana JF huyu .
Mbona unakurupuka hivyo tena? Kuuliza yuko wapi ina maana ngapi? Hiyo hoja iko wapi? Haya mie sio wa JF lakini nimo humuhumu na sing'atuki!

Alikuwa na maana gani ya kuanzisha hi thready...halafu anagwaya?
Ngoja niangalie kama hii ni mwenendo wa humu manake mtu ukiwa mgeni basi kila mtu anakutupia madongo shabash.

Sasa lunyungu unataka kumtetea kama sio msemaji wake tena?
 

=SYLLOGIST punguza hasira mkuu wewe kata issue tuu hakuna cha ugeni wala nini, ugeni kwani leo ndio umeingia duniani na wewe? Poa kata issues, bring syllogistic argument.

Haya kanyaga twende mwanangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…