Ndesamburo alivyowaaga wananchi kwa kuwaachia soko la kisasa

Bahati furaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
3,054
Reaction score
1,415
Ndesamburo alivyotumia Sh1b kutoa ajira kwa vijana 1,000
Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, anaweza kuingia katika vitabu vya kumbukumbu kutokana na staili yake ya kuuaga uwanja wa kisiasa kwa kutazama tatizo la ajira kwa vijana, ambalo ni tatizo sugu na limekuwa likizungumziwa kisiasa kama bomu linalosubiri kulipuka.

Alipowaaga wananchi wake kwa kuwaachia kitega uchumi chenye thamani ya zaidi ya Sh1 bilioni.
Ndesamburo, amekuwa mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo; yaani kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 na sasa ametangaza rasmi kutogombea ubunge.

Hoja hapa siyo kustaafu ubunge, ila ni staili aliyoitumia kustaafu pale alipoamua kujenga soko la kisasa na kuliita "Kiborlon Shopping Centre" na kuwapa hisa wafanyabiashara kadhaa wadogo, maarufu kama Wamachinga.

Ndesamburo anasema amejenga soko hilo kubwa kuliko yote katika mikoa ya Kaskazini, kama njia ya kutatua tatizo la muda mrefu la wafanyabiashara wadogo na kati. Soko hilo lina runinga kubwa katika mlango wake mkubwa ikiwa na stesheni mbalimbali za televisheni na lina vibanda zaidi ya 200 vya maduka na eneo la kuchukua "Machinga" na wauza mitumba 1,000.

Ujenzi wakwepa fitina za kisiasa

Ndesamburo anasema isingekuwa rahisi kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kujikusanya na kuchanga fedha za kujenga soko hilo la kisasa.

"Tatizo la maeneo ya kufanyia biashara kwa Machinga na wafanyabiashara wa kati ni kubwa sana na nilipokuwa mbunge kwa mara ya kwanza mwaka 2000 niliahidi kushughulikia tatizo hili," anasema.

Anasema alibaini Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakati huo ikiongozwa na CCM, ilikuwa haina mpango wa kutenga eneo kwa ajili ya Wamachinga na kwamba hata mikakati iliyowekwa ilikuwa ni ya muda na haiwasaidii wengi.

"Hapo ndipo niliponunua eneo hili na kutoa wazo kwa Serikali kwamba kwa kupitia mpango wa PPP (ubia serikali na sekta binafsi) tujenge soko la kisasa la Mitumba na Machinga," anasema Ndesamburo.

Ndesamburo anasema wazo lake hilo lilikataliwa na viongozi wa Serikali ya CCM kwa sababu za kisiasa kwamba kama kungejengwa soko la wafanyabiashara hao, basi jina lake lingepanda chati.

"Kwa sababu ya vita kubwa ya kisiasa ndani ya Jimbo letu nikaamua nijenge mwenyewe lakini swali likawa je, hawa madiwani wa CCM wangekubali kunipitishia michoro ya soko?" Anasema akifafanua:

"Nikachora ramani na ikapitishwa kwa jina la mhindi. Sikutumia jina langu kwa sababu kama ningelitumia wasingekubali," anasema Ndesamburo ambaye pia ni mfadhili wa Chadema.

"Nilipoanza kutaka kujenga, usalama wa Taifa, Gama na Manispaa wote walikuja hapa kuzuia nisijenge lakini wakati huo tayari nilishakuwa na vibali vyote vya ujenzi kwa jina la Mhindi."

‘Vita vya panzi'

Ndesamburo alidai pamoja na soko kukamilika, lakini wapo makada wa CCM ambao wameshika vyumba vya biashara lakini hawavifungui ili dhana ya kuwapo kwa soko isiwepo.

"Nimesema yeyote asiyefungua tutawapa watu wengine. Yeyote ambaye hata kama amelipa deposit (dhamana) tunamnyang'anya na tutakata fedha yetu ya kukodisha," anasema Ndesamburo.

Mbunge huyo anasema ametoa ‘ofa' kutoka sasa hadi Julai Mosi, mwaka huu, wafanyabiashara waliochukua maeneo ya biashara katika soko hilo wafanye biashara bure na baada ya hapo ndiyo wataanza kulipa kodi.
Ndesamburo anasema wafanyabiashara wote watakaomuunga mkono kwa kufungua biashara zao kuanzia jana, watakuwa wana hisa wa soko hilo ili kuondoa propaganda chafu alizodai zinaenezwa na CCM.

"CCM wanapita huko na huko wanasema hiki ni kitega uchumi cha mtu binafsi lakini mimi nasema hawa waliokodi vibanda hapa watakuwa wanahisa. Tutaendesha pamoja hili soko," anasema.

"Siyo hivyo, lakini nimeamua kuagiza mitumba moja kwa moja kutoka Ulaya kwa wafanyabiashara watakaotumia soko hili. Bei yake itakuwa chini ya wanaonunua hapa nchini."

Kodi ni mzozo

Pamoja na ofa nyingi zilizotolewa na Ndesamburo baadhi ya wafanyabiashara, wanaona kodi ya Sh100,000 kwa mwezi kwa vibanda katika soko hilo ni kubwa na kutaka ipungue hadi Sh50,000 kwa mwezi. Hamisi Shemdoe ni mfanyabiashara wa kutembeza viatu na anasema anatamani kukodisha kibanda, lakini hawezi kumudu kodi ya Sh100,000 kwa mwezi labda angepewa kwa Sh30,000 au 50,000.

Hata hivyo, Ndesamburo mwenyewe anasema milango ya majadiliano haijafungwa, hivyo wale wenye maoni na michango ya namna ya kuboresha huduma za soko hilo, wako huru kumuona.

Pamoja na mipango hiyo, watu wengi wana wasiwasi kwamba chokochoko za kisiasa zinaweza zikakwamisha uzuri na shughuli za kibiashara katika soko hilo.

Hayo yanazungumzwa huku kukiwa na imani kwamba kwa kuwa soko hilo limejikita kwa faida ya jamii, siasa kamwe hazina nafasi.

Chanzo: wenzetete blog
 
dah kweli uyu mwandishi aliye andika kapanga vizuri habari hii utamu mwanzo mwisho
 
laki si pesa umekula like yangu
Ila hawa masisiem wanakwamisha sana mipango ya wapinzani
 
Last edited by a moderator:
Ndesamburo ni sawa na mawaziri 20 wachovu...
 
Kodi 100000 kwa mwezi ? Kwa navyo jua biashara moshi ilivyo ni hela nyingi sana kwa sababu hizo nguo zinatembezwa sana moshi kutoka Maimoria kwa hiyo ushindani wa hao jamaa utakuwa juu sana.
 
Kodi 100000 kwa mwezi ? Kwa navyo jua biashara moshi ilivyo ni hela nyingi sana kwa sababu hizo nguo zinatembezwa sana moshi kutoka Maimoria kwa hiyo ushindani wa hao jamaa utakuwa juu sana
Ndesa mwenywe kasema milango ya majadiliano kuhusu kodi haijafungwa.
 


Hilo soko/genge mbona hatulioni, camera zenu mbovu?
 
Tungelipata wabunge wenye moyo na uzalendo kama huyu Baba, bila shaka majimbo yote na wananchi wake wangeiishi kama wapo eponi.

Tatizo la viongozi wetu wanaweka mno mbele Siasa kuliko maslahi ya wananchi.

Rais JK aliahidi kujenga Machinga Complex kila mkoa, lakini kwa kuwa ni kiongozi wa CCm hakuna aliyepinga wala kuwa na shaka.

Lakini kwa Ndesa kwa kuwa ni kiongozi wa upinzani watu wa CCm pamoja na serikali hawapendi jambo hili lifanyike na kuanza kuhusisha na Siasa.

Tutafika lini sisi Watanzania kule kwenye Ardhi inayotoa maziwa na Asali????


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ndesa mwenywe kasema milango ya majadiliano kuhusu kodi haijafungwa.

Hata kama mkuu kwa maisha ya moshi nayoyajua mim hilo hiyo ni nyingi sana ukizingati kuna soko la mitumba miomoria kwa sasa ambalo litaaongeza ushindani mkubwa kwao na akipinguza sana sio zaidi ya elfu 20/30 hivi . Na kumbuka mtu wa kipato Cha kawaida anaweza kukaa hata miezi 4/5 bila kununua nguo . Hii itakuwa changamoto sana kwao
 
Nimecheka sana Etiliyumia jina la Mhindi ccm wakapitisha mchoro.
 
Kwa Maeneo yale Bei kubwa.
Sasa mazungumzo yapo kwani ule ni mdana?

Aseme tu nimeshusha bei kwa kiasi fulani.Angeanza na elfu 50 kisha kama miaka miwili baada ya eneo kuvutia ndio akaongeza.
Mzunguuko wa pesa inategemea na watumiaji wa huduma.Na ushindani wa biashara maeneo karibu na yale.

Nenda Kariakoo pale uone watu wanavyolia shimoni mle hali ilivyo ngum
 

Nikikuambia ukusanye 50'000 hadi ufikishe amount iliyotajwa hapo itakuchukua miaka mingapi?
 
Hii habari aliyeandika yuko balanced sana. Safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…