Ndesamburo anunua helkopta za kampeni Chadema

kwani CHADENA ikisaidia albino ni NGO?
CCM wameshafulia wametulia hela zetu tunataka kuona vyama vya upinzani vitumie pesa kwa utaratibu mzuri.

mojawapo ya utaratibu mzuri ni pamoja na kujipatia viongozi mbalimbali ambao wanaweza kutekeleza sera hizo za chama, siyo?
 
mbona watu mnakua warahisi sana kuitetea CHADEMA by any means? tusemeni ukweli panapobidi kama kweli mnataka kujenga nchi yetu mpaka sasa CCM 0 upinzani 0
bado mnataka kuforce kingi?
 
mbona watu mnakua warahisi sana kuitetea CHADEMA by any means? tusemeni ukweli panapobidi kama kweli mnataka kujenga nchi yetu mpaka sasa CCM 0 upinzani 0
bado mnataka kuforce kingi?

Sidhani kama ni makosa kutetea wanachokiamini by any means.
 
hatuwezi kuwa na imani kwa watu ambao hapa mwanzo tu wanachemsha, mfano kuvunja demokrasia kwa kumzuia Zitto na kutumia pesa vibaya...nataka kuona mambo tofauti na CCM......ndo mana mimi pendekezo langu ni kuunda chama kipya bas ambacho kitawakilisha watanzania wote
 

Na huyo unayetaka akuanzishie chama kipya ni ..............???
 
Sidhani kama ni makosa kutetea wanachokiamini by any means.
NA SISI PIA WENGINE TUNAAMINI THEY R WRONG BY ANY MEANS...sijawahi kuona watu wakikosoa upinzani humu ndani sebreni kila ;CHADEMA] wanachofanya wako sahihi...mmh inanitia mashaka sana
 
NA SISI PIA WENGINE TUNAAMINI THEY R WRONG BY ANY MEANS...sijawahi kuona watu wakikosoa upinzani humu ndani sebreni kila ;CHADEMA] wanachofanya wako sahihi...mmh inanitia mashaka sana

Si kweli. Hujawahi kuona may be kwa kuwa haujatafuta na kuona, au basi haujabahatika kuona tu.
 
NA SISI PIA WENGINE TUNAAMINI THEY R WRONG BY ANY MEANS...sijawahi kuona watu wakikosoa upinzani humu ndani sebreni kila ;CHADEMA] wanachofanya wako sahihi...mmh inanitia mashaka sana

Hiyo ni kweli lakini huwezi kulazimisha watu kuwa na mtizamo kama wa kwako. Hiyo ndiyo demokrasia. Wewe kama unaona ccm wako sawa kuna wengine wanaona vinginevyo. The same thing kwa chadema, cuf nk
 
NA SISI PIA WENGINE TUNAAMINI THEY R WRONG BY ANY MEANS...sijawahi kuona watu wakikosoa upinzani humu ndani sebreni kila ;CHADEMA] wanachofanya wako sahihi...mmh inanitia mashaka sana
Selective retention and perception....You remember only whay you want to remember....Hata mjadala huu ukifuatilia kwa makini utagunduwa kuwa madai yako bado hayana ukweli.
 
Kula tano mwanangu Ndesa najua nitaitumia mwakani nikiwa mgombea ubunge wa chadema
 
Ni much better kununua helicopter kuliko kukodi. Kama Yeye akiikodisha kwa chama cheke itakuwa vizuri pia. Lakini ni mawazo finyu na ni mawazo ya kikomunisti kusema kuwa haifai kununua chopa kwa kuwa ni kufuja pesa.

CCM nao wanaweza kununua maana Rostam na Lowassa are rich enough to buy a couple of Helis. Cha muhimu ni kuwa wasituibie hela zetu, kama ni zao za mifukoni au za vyama vyao wanunue tu.
 
halafu watoto wake, wakweze wakipewa viti maalum mtalalamika?

Hata TANU ya Nyerere wakati inajijenga miaka hiyo ya kugombea uhuru ilifadhiliwa na akina Rupia na wengine kwani ni nini kilifuata baada ya uhuru na TANU kukua? Hata mzee Songambele alifadhili lift ya tipper la mchanga kwa mwalimu toka PUGU secondary akija Lumumba! Haya mabo ya kawaida sana ndani ya vyama na yapo duniani kote. Wafadhili kwa vyama vyote sawa sio kwa CCM sawa kwa CHADEMA haramu.

Tuulize ule ufadhili wa kuchota kodi zetu kwa ufisadi halafu zinapelekwa kwa CCM
 
Hiyo ni kweli lakini huwezi kulazimisha watu kuwa na mtizamo kama wa kwako. Hiyo ndiyo demokrasia. Wewe kama unaona ccm wako sawa kuna wengine wanaona vinginevyo. The same thing kwa chadema, cuf nk

sijasema kuwa CCM wapo sawa, mpaka sasa CCM 0 upinzani 0, ila tukipata chama bora ambacho kitamwakilisha kila mtanzania itakua CCM 0 upinzani 1...lakini kwa sasa chama tawala tulicho nacho hakina dira ya maendeleo, na upinzani bado hawapo kikamilifu..chakufanya ni kuunda chama kipya tu..au alternatively kujikita saana kwemye ubunge
pia vyama hivi vituonyeshe mfano ambao uwe tofauti na CCM na si kurudia madudu ya CCM
 

unajuaje kama ndesa ajaiba pesa za wananchi? nikisema kuwa helkopta si ya muhim, napima mizani mkuu...lipi bora kujenga shule ya albino au kununua helkopta...tena basi hiyo ya kujenga shule kwa walemavu ingekua na impakt kuliko hata helkopta ambapo inaweza isizae kiti cha ubunge huko inapotumika kuliko ukijenga shule moja kwenye mkoa mmoja for sure unapata ubunge kwa ticket ya CHADEMA
 
tunachotaka ni utumiaji wa fedha kwa usahi najua hata ulaya watu wanafanya fund raising kupata pesa za kampani na wengine wanakopa, lakini wanazingatia sana idadi ya pesa watakayo tumia....for me kuna mengi chadema wanatakiwa kufanya kuliko kununua helkopta...me metoa mfano wa shule za abino na ndo naung'ang'ania huo kwani ndo jambo linalo ikumba taifa kwa sasa.......
 
Ndesamburo anunua helkopta za kampeni Chadema
Mbunge wa Moshi Mjini,Philemon Ndesamburo(Chadema), amenunua helikopta mbili za kampeni.
*Zitaanza uchaguzi wa serikali za mitaa Â
Boniface Meena, Moshi
Â
MBUNGE wa Moshi Mjini,Philemon Ndesamburo(Chadema), amenunua helkopta mbili kwa ajili ya kukisaidia chama hicho katika kampeni za chaguzi mbalimbali hapa nchini.
Â
Moja ya helkopta hizo tayari iko hapa nchini na nyingine itawasili Jumatatu (kesho) na tayari mbunge huyo ameshapata vibali vya kuziruhusu helkopta hizo kutumika hapa nchini.
Â
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Ndesamburo alikiri kuwa amenunua helkopta hizo, ili kukipunguzia chama chao gharama kubwa za kukodi wakati wa kampeni.
Â
Hatua hiyo ni kubwa zaidi kwa Chadema, chama ambacho kimekuwa kikijitahidi kujiimarisha na kuongeza nguvu hasa wakati wa uchaguzi.

Tangu mwaka 2005 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Freeman Mbowe alipogombea urais kwa mara ya kwanza, chama hicho kilitumia helkopta ya kukodi.

Hata katika baadhi ya chaguzi ndogo za ubunge zikiwemo za jimbo la Busanda na Tarime, chama hicho kilitumia helkopta za kukodi kwa ajili ya kufanyia kampeni.

Lakini safari hii, chama hicho kimeamua kumiliki helkopta yake huku Ndesamburo akisisitiza: “Vibali vyote nimeshapata kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga na vile vile vya kuitoa hiyo moja Nairobi na kuifikisha hapa Jumatatu”.
Â
Alisema kuwa helkopta hizo zitaanza kufanya kazi katika kampeni za serikali za mitaa katika majimbo yote ya Mkoa wa Kilimanjaro na baadaye katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Â
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana ni kuwa Chadema imesimamisha wagombea zaidi ya robo tatu katika kila jimbo mkoani Kilimanjaro.
Â
Katika Jimbo la Moshi Mjini, chama hicho kimesimamisha wagombea 60Â na Jimbo la Rombo kimesimamisha wagombea 52.
Â

Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo huku idadi ya wapigakura ikiwa ndogo kinyume na matarajio.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya vyama kujipanga kikamilifu ili kuhakikisha wanakwepa kile wanachoita hujuma dhidi ya CCM.

Uchaguzi huo ni muhimu kwa vyama vya siasa kujipatia mtaji na kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambao unatarajiwa kuwa na mchuano mkali.


Viongozi wa serikali za mitaa wana nguvu na ushawishi mkubwa wa kimaamuzi katika uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais, kwani wapigakura wengi wako kwenye maeneo yao.

Pia ngazi ya uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu katika maamuzi ya maendeleo ya nchi kutokana na watu wengi kuishi vijijini ambako pamoja na mambo mengine kuna shughuli nyingi muhimu za uchumi hasa kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa taifa.

Inategemea unaangalia nini; kama helikopta zitasaidia kupata wawakilishi wengi mitaani ambao wataweza kutekeleza agenda za Chadema.. basi kuwekeza huko kunalipa. Siasa ni pamoja na kuwekeza katika kugharimia nafasi za kisiasa na hakuna nafasi za kisiasa ambazo ni bei chee.

la maana ni kuona jinsi gani uwekezaji huu utalipa. Hili litaoonekana baada ya matokeo ya uchaguzi. Na hapo ndipo tunaweza kwa haki kuhukumu kama ulikuwa ni uwekezaji makini. Lakini vile vile.. kwenye maeneo mengine yawezekana hizo Helikopta zikatumika katika mambo mengine zaidi ya kampeni za kisiasa. Fikiria.



Na njia mojawapo ni kupata wawakilishi au viongozi kwenye mitaa wanayoishi walemavu hao..
 

inaelekea hujui malengo ya chama cha siasa ni nini.sasa kwa taarifa yako kusaidia walemavu sio moja ya malengo ya chama chochote cha siasa na usifikiri watu watakupigia kura kwa kusaidia walemavu kuliko kueleza sera zako na kuwafikia wananchi kuwa[a elimu ya sera zako ikiwemo hao walemavu wanaoishi katika mazingira magumu
 
Nimeipenda hii line of thought, na ingekuwa bora kuiangalia vizuri. Swali la Ufadhili wa vyama vya siasi ni muhimu sana katika nchi inayofuata mfumo wa demokrasia. Ishu inakuja hasa kwenye swali la wafadhili na remuneration. Mara nyingi wafadhili watapenda kupata something in return na ndio kilicholeta hili swali la kwanza....
halafu watoto wake, wakweze wakipewa viti maalum mtalalamika?

Jibu la Balantanda ni zuri lakini limeacha mengi wazi...
Itakuwa ngumu sana kumlalamikia mfadhili aisee.Ni sawa na CCM wanavyowaonea haya mafisadi(wengi wao ni wafadhili wa chama).....

Kwa mfano: Je ni haki ya mfadhili kuwa remunirated? Na kama ni haki/sawa, ni remuniration gani inayokubalika?
Umejibu swali kwa kusema jirani(CCM) anafanya, hivyo ni haki kwa Chadema nao kufanya hivyo. Okay...Lakini katika jibu umeingiza neno UFISADI. This takes the conversation katika direction nyingine.
Kwanza, kwangu mimi neno UFISADI = the use of public funds for private benefit. Hivyo katika jibu lako, ume-imply kuwa ni haki kuwarudishia Wafadhili chao hata kama itafikia kiwango cha kuwapa Mali ya Umma. Nadhani hapo tunakuwa tumevuka mpaka. Kuendesha vyama vya siasi ina cost kubwa, na ndio maana kila chama kina power base yake, ambayo kwa mara nyingi ndio wafadhili wao. Kwa mfano katika nchi zilizoendelea kisiasi, unakuta chama chenye policies za kibepari huwa na wafadhili wengi kutoka watu wa business class - yani watakao faidi matunda ya policies za chama. Hivyo hii relationship kati ya Chama na Wafadhili inakuwa ipo katika level ya 'strach my back and i will scratch yours'. Lakini relationship hii inafikia kikwamo pale Chama kitakapotumia Mali ya Umma katika kuwa-remunerate Wafadhili. Nadhani jibu la MWJJ limeongelea hichi:

 
elewa kwanza ndo ukoment mkuu
nimetumia kigezo hicho cha albino kuwa ndo current problem ya TZ kuliko helkopta
kila chama cha upinzani kina sera nzauri tatizo kuzitekeleza
Mbona chadema ni chama cha demokrasia lakini ndani hamna demokrasia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…