Ndesamburo anunua helkopta za kampeni Chadema


Hivi mimi na wewe anayeongea PUMBA ni nani, Una pointi Nzuri sana Kichwani mwako lakini Badala ya Kuongozwa na Dhamira safi kuzitoa Unaongozwa na Hisia Zako tena Hisia za Chuki dhidi ya Wachaga, Mkuu Nunua zako basi upeleke kusini.

Ni wapi Pameandikwa kwamba ni Mali ya CHADEMA?
 

Nahisi hujanielewa na unahitaji kusaidiwa....hoja uliyoitoa hapa ni kuwa Helkopta ni mali yake na ofcoz kama hivyo ndivyo basi aendelee na anachotaka kufanya....lakini kama amenunua huduma hiyo kukisaidia chama chake ambacho kwa mujibu wa sheria za usajili wa vyama vya siasa kinapaswa kiwe na uwakilishi wa mikoa yote ya Tanzania ikiwemo visiwani...Basi si sahihi kwa yeye kukisaidia chama huku akiweka masharti namna MSAADA HUYO utakavyotumika na suala la wapi chomo hicho kitafanya kazi kinamaana kubwa sana katika DURU za kisiasa.

Mkuu usitake nihoji uwezo wako wa kuchambua mambo, au umesahau tupo kwenye jukwaa la siasa na si kwenye MIPASHO? Mi sina chuki na wachaga kwanza ni shemeji zangu, ila najaribu kutoa mawazo yangu hasa kwa faida ya wanachadema maana huwezi kujua kinaweza kuwa chama dola na kushika mustakabali wa maisha yetu....unalooooo weweeee?
 

Unajua Mkuu MIPASHO ni Pamoja na Umbeya au UONGO ni Masharti gani hayo mkuu.

Straight to the Point Mkuu haina haja ya kuandika mistari zaidi ya Mitatu
 


As you requested...anything else?
 

Uchagani inawezekana unakusikia tu,kisiasa wengi wa wananchi wa kule ni waelewa,miundo mbinu pia si mbaya sana na hivyo kuwafikia wananchi si tatizo kubwa,na pia asilimia kubwa ya wananchi wa huko ni well informed kwa taarifa yako.
Nashangazwa unapozungumza kama mtoto mdogo et zitaanza kutumika uchagani,kana kwamba zimenunuliwa kwa ajili ya kuwafurahisha wachagga,kuwabeba kwenye helicopta ama kuwaonyesha helicopta,ndivyo unavyo imply,jambo ambalo sidhani kama ni malengo yao....Na kamwe hayawezi kuwa malengo ya mtu mwenye akili timamu.
Nadhani hizo ni asset zitakazosaidia shughuli zao za kichama na kama ni kuwafikia wananchi kwa Helicopta sidhani kama Kilimanjaro kuna tatizo la kuwafikia wananchi kwa urahisi kwani miundo mbinu ni mizuri....Na kwahivyo basi maoni yako ndio yamejaa ukabila wa kufikirika. Unalazimishia ukabila ambao haupo.
 
As you requested...anything else?

Mkuu kwa hiyo Tatizo lako ni Helicopter za Ndesamburo Zitaanzia Wapi, Kwa Hiyo kwa Sababu zinaanzia Mkoa wa Kilimanjaro ( Ambao una Kabila Zaidi ya Wachaga) Basi kuna Ka element ka Uchaga

Nijibu Swali Hili Mkuu

Uchaguzi wa 2005 Chopper ya CHADEMA ilianzia wapi vile?

Asante
 


Wewe bila shaka unahitaji msaada wa kitaalam zaidi.....Hoja yangu iko hivi, hakuna asiyejua kuwa CHADEMA imejijenga sana huko juu, ingekuwa busara kama wangetumia rasilimali hiyo kujenga ngome nyingine ya kushambulia mwaka 2010. Ni sawa na Tajiri anaeamua kumsaidia tajiri mwenzie labda anajua atafaidika pia.

So if you want to continue with your silly debate be my guest. My point is not chaga people rather sharing of part cake equally kama ilivyotakiwa gawiwo la ruzuku ya chama hicho ambacho robo tatu ya wabunge wanatoka huko na kalibia wabunge wote wa viti maalum nao wa huko huko ukimtoa Mhe. Mhonga.

Zaidi ya hapo, nitakuona ni MGOGORO tu.
 


Pamoja na ukweli kuwa umevamia mjadala kwa ushabiki...nakushukuru kwa kunisaidia kuwasilisha hoja yangu kwa urahisi zaidi....kama nilivyohighlight sentensi zako....kwanini aamue kutumia helkopta huko wakati inaeleweka supposely wachaga ni waelewa na wasomi...one more thing miundo mbinu iko tambarare?

Usiingilie mambo kwa jazba fanya tathmini kabla ya kuja kuonekana mwingi wa ukabila na kwa jinsi ulivyotetea...sichelei kusema wewe mwenyewe ni MCHAGA hivyo si JAJI sahihi wa mada hii.
 

Siko hapa kujudge ila kuchangia,na hakuna nilipoingilia anything kwa any jazba "Wingi wa ukabila" Unaozungumzia wewe mbinu yako kwenye mjadala huu,kwa kuni identify kutokana na jina langu,je na mimi nikiku disqualify kwa kujiita "FiksiMan" Utajibu nini? Wewe ni FIKSIMAN hivyo si JAJI sahihi wa mada hii...
 

asante kiongozi kwa majibu yako mwanana...kweli kuwa na akili ni pamoja na kujua kuzitumia
 
ufisadi huo, what goes around comes around twice
 
Hence, the issue is not which party is the ruling part (it may be CCM, CHADEMA, CUF, u name it...) but rather the issue is what is the composition of national assemply?

As I said several times, I love ruling party to have 60% to 70% maximum and opposition 40% to 30% minimum.

"CHADEMA when become the ruling part will behave like CCM at least by 75%"

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kama ule mkakati wa RAIS WA KABILA YETU wa mwaka 1995 wameuacha, tutawaunga mkono. Vinginevyo acha wanunue vitendea kazi na hasa baada ya jaribio la Zitto kuwa limezimwa kiaina.
 

Napenda watu wanaokwenda Straigth to the POINTI ndiyo maana nawapenda Wahandisi na Sayantisti

2005 CHOPPER ILIANZIA WAPI?
 
Itakuwa ngumu sana kumlalamikia mfadhili aisee.Ni sawa na CCM wanavyowaonea haya mafisadi(wengi wao ni wafadhili wa chama).....

kama wengi wao ni wafadhiri wa chama watakuwa wanaogopa kukemea maovu yao
 
Nafikiri huyo mzee kama kweli anataka kuki imarisha chake ni vizuri akaanza kukifadhili chama chake kuanzia ngazi za nchini!sina uhakika sana ni mikoa mingapi chadema wana usafiri wa gari,lakini kwa uelewa wangu wa baadhi ya mikoa chadema haina hata ofisi achilia mbali usafiri wa watendaji wake!ni vizuri hizo pesa za helkopta angewanunulia watendaji wa mikoa magari au hata piki piki waweze kufanya kazi zao kiufanisi zaidi!

Uendeshaji wa hizo helkopta zina gharama sana pia zitatumiwa kwenye kampeni baada ya hapo zitasimama tu!Kuna mtendaji mkuu mmoja wa Chadema alifanya ziara mkoa mmoja alipelekewa kusaini kitabu cha wageni hotelini kwa kuwa mkoa huo hauna ofisi!!!

Chadema ikiwa wanataka kukiimarisha chama chao ni bora wawe na vitendea kazi kuanzia wilaya mpaka mikoa!Viongozi wakuu wanatumia usafiri wa Helkopta huku katibu wa wilaya au mkoa hana hata baiskeli kuwafikia wanachama wake au hata wapiga kura!!!Watendaji hawana hata chumba cha ofisi kufanyia kazi za chama sijui huwa wanawasiliana vipi na makao makuu ya chama chao!au wanatumia Simu za Mikononi na sms!!!
 
Wakuu ile programme ya online registration and support iko wapi? Chadema tupeni upadates please. Tuna hamu nayo
 
ufadhilii wa aina yeyote huwa na fadhila zake toka enzi na enzi..

cha muhimu fadhila hizoo ziwe za kujenga na sio kubomoa..

John Rupia msaada wake kwa nyerere sina uhakika ulisaidia kumfikisha Paul Rupia kuwa Katibu wa Ikulu!!!!!

Famila za akina sykes, tambaza,mtevu, na wenzaoo katika mapambano ya uhuru zilifaidikajee??

Juhudi za Ndesa na maendeleo ya Chadema hazina kipimooo...anafaidikajee???
 
NDIYO, NIKIPATA NAFASI NYINGI NITAKUWA NA USEMI NA HIVYO IWE RAHISI KURUDISHA GHARAMA NA KULIPA MADENI NILIYOSHIRIKIANA NA WANZANGU KUKOPA TANGU 2000! Hili linaweza kuwa jibu rahisi na linaloeleka zaidi, kinyume ya hilo tanadanganyana. Baada ya chaguzi itafuata falsafa ya "IT'S OUR TIME TO EAT" Huu siyo ukombozi ni upotevu wa raslimali usio na tija kwa jamii hii maskini. Uendeshaji wa siku moja tu wa helkopita moja utaufanya ukoo wako ukuthamini kwa msaada wa maana sana kuuendeleza, fikiria tena!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…