Ndesamburo anunua helkopta za kampeni Chadema



hata kwenye kampuni mwenye hisa kubwa ndio mwenye sauti ati. . . .
Muhimu kusiwa na nia mbaya katika ufadhili huo. Ndio maaana hata mabalozi wetu wakikohoa mkulo anatetemeka. Money talks bwana. . .
 
elewa kwanza ndo ukoment mkuu
nimetumia kigezo hicho cha albino kuwa ndo current problem ya TZ kuliko helkopta
kila chama cha upinzani kina sera nzauri tatizo kuzitekeleza
Mbona chadema ni chama cha demokrasia lakini ndani hamna demokrasia?

Nafikiri una-matatizo kidogo kwenye kuprocess taarifa....yani huelewi kabisaaaaaa! Naona error code tu kwenye posts zako, hamna kitu.

Fisadi ni nani? Ndesa yupo kwenye list yako a mafisadi??---- mfanyabiashara ambaye hana record chafu

CCM ilinunua magari (walifadhiliwa na mafisadi)- Mahandra kutoka India kwenye kampeni za 2005, magari kibao tu, kila wilaya nafikiri ilipata gari mbili. Kwa nn wasingejenga health centres au hata dispensaries vijijini? haikuwa kazi yao, hiyo ni kazi ya serikali......kama chama, wanahitaji kujiimarisha.

kama hujaelewa mpaka hapo sijui tukusaidiaje!
 
huu nao ukweli eti. think people, think.

kwa hiyo chama kiendeshwe kwa fedha ya kadi sh 1000 sijui? au wafadhili wawe nguruwe kwasababu hatuwezi kuwapa nafasi za upendeleo, labda tuwale tu!!

do you have problems with thinking?
 

Ndesa amenunua helikopta yake hajainunulia CHADEMA helikopta. Amenunua helikopta kwa ajili ya kufanya biashara. Hamna Commercial company hapa Tanzania ya kukodisha helikopta, hii ya Ndesa ndio ya kwanza. Ilikuwa ukitaka kukodisha helikopta lazima uende SA au Kenya, na rates zina double unapoitoa nje ya nchi.

Wakati wa kampeni Ndesa anaweza aitoe bure kwa CHADEMA au aikodishie kwa bei nafuu. Helikopta inaingia leo, zimebaki siku chache za Kampeni hiyo helikopta itafikaje huko Kusini? Hata angependa kwenda huko logistics zinagoma.



Ndesamburo ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro. Priority yake ya kwanza kama mwenyekiti wa mkoa ni kujenga chama katika mkoa wake. CHADEMA kina mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa kutoka Kilimanjaro. Ni busara zipi hizo unazozizungumzia?



Kwa taarifa yako wabunge wa kuchaguliwa wa CHADEMA ni mmoja tu ambaye ni mchagga - Ndesamburo. Arfi anatoka Mpanda, Mwera anatoka Tarime, Zitto anatoka Kigoma na Slaa anatoka Karatu. Kwa viti maalum - Halima Mdee sio mchaga, ni Mpare na Mama Maulidah Komu alikuwa mgombea mwenza kwa tiketi ya urais 2005. Hivi mpaka leo bado hujui kuwa mgombea mwenza lazima awe anatoka visiwani? Au utasema Tume ya uchaguzi iliipendelea CHADEMA?


.
 
Wakuu ile programme ya online registration and support iko wapi? Chadema tupeni upadates please. Tuna hamu nayo

Namba ni 15710. Sasa hivi inafanya kazi kwa mitandao ya Zain na Vodacom. Tigo na Zantel wataunganishwa baada ya muda sio mrefu.



.
 
Namba ni 15710. Sasa hivi inafanya kazi kwa mitandao ya Zain na Vodacom. Tigo na Zantel wataunganishwa baada ya muda sio mrefu.


.

Kampeni zenu mnaanza lini kwenye huu uchaguzi serikali za mitaa?? sijawaona kabisa, mitaani naona wale wa kijani wanapepea, vipi tupe programme tuwaunge mkono hiki ndo chama mbadala.
 
Ndesamburo tangu zamani hajaonyesha kusaidia watu wake kiufisadi. Wagomvi wake ndio wanadai hayo ya ufisadi. Kila kilicho chema kina gharama. Kama tunataka TZ iwe na vyama mbadala vyenye nguvu ni lazima watu kama kina Ndesamburo wawepo ilhali wanao uwezo kusaidia. Sasa na kina nanihii (Bajaji?) wanaochota pesa ya umma na kuipeleka mabenki ya nje, ndio sampuli tuitakayo?

Ubarikiwe tu Ndesamburo, kelele za wapita njia hazimnyimi usingizi mwadhini.

Leka
 
UNAVYOMTETEA HUYO NDESAMBURO SIYO FISADI, JE SIKU MAFILE YAKE YATAKAPOTOKA NA KUJULIKANA YEYE NI FISADI UTASEMAJE?
ACHA USHABIKI KIJANA
NANI ALIJUA KUWA MENGI KAKOPA MIAKA HIYO HELA ZA WANANCHI MPAKA LEO AJARUDISHA?
ME KWA NDESA KUWA NI FISADI AU SI FISADI SIWEZI SEMA LOLOTE KWANI WATU TULIOWAFIKIRIA KUMBE SIO NA TUSIOWAFIKIRIA KUMBE NDIO WENYEWE

KUHUSU TYPING ERROR computer yangu imeingia kirusi

teh teh thh thh teh
 

JF imejaa viroja kweli.

Kukopa pesa ni ufisadi? Yaani so far hiki ndicho ccm mnaweza kuja nacho?

Kwamba ccm inaiba pesa za wananchi --- mzee chenge ni kiongozi wa juu kabisa wa ccm --- inalinganishwa na mwanaccm mwingine (mengi) aliyekopa na akachelewa kurudisha?!
 

Tuache kupanga bajeti ya fedha zilizo kwenye mifuko ya watu wengine.
Sisi fedha zetu tumezitumiaje kusaidia hao albino wapate walau kikombe cha chai bila mkate kila asubuhi? Au hata hicho kikombe kimoja cha chai ni aghari sana kwetu?
Matumizi mazuri ya fedha ni kutatua matatizo yanayoonekana? au ni kung'oa mzizi wa kuyaneemesha matatizo?
Walemavu wanaoishi kwenye mazingira ya shida watasaidiwa tu endapo mfumo uliopo utatupwa jalalani na jamii yote kukubali kwamba matatizo mengi tuliyo nayo ni matokeo ya uhalibifu wa makusudi wa taratibu za kiserikali na kijamii tulio ulea na kuuenzi kwa miaka mingi sana.

Mshangao wako ni sawa na kumshangaa mkulima akifukia gunia zima la mbegu za mahindi na maharage ardhini kwa kisingizio cha kuzipanda wakati wa msimu wa kilimo huku familia yake ikishindia uji tu. Kwa nini asipike kande kile akiitacho mbegu ili wanae wajichane na kujaza matumbo yao??
 
mengi sio kama kakopa kachelewa, ni HAJARUDISHA MKOPO MPAKA SASA
mimi siisemei CCM wao wamesha chemsha kwenye hilo swala la ufisadi
kuhusu ndesa vyanzo vyake vya mapato hatuvijui so tukae kimya kuliko kumdeclare sio fisadi..
 
mengi sio kama kakopa kachelewa, ni HAJARUDISHA MKOPO MPAKA SASA
mimi siisemei CCM wao wamesha chemsha kwenye hilo swala la ufisadi
kuhusu ndesa vyanzo vyake vya mapato hatuvijui so tukae kimya kuliko kumdeclare sio fisadi..
Mzee Ndesa si fisadi.
Welcome to JF Semenya naona umejiunga juzi juzi tu.
 
mengi sio kama kakopa kachelewa, ni HAJARUDISHA MKOPO MPAKA SASA
mimi siisemei CCM wao wamesha chemsha kwenye hilo swala la ufisadi
kuhusu ndesa vyanzo vyake vya mapato hatuvijui so tukae kimya kuliko kumdeclare sio fisadi..

Mkuu Semenya vipi tena?

Mbona unaamuru watu hapa cha kusema na/au cha kutosema? Kwa nini unataka maoni yako ndiyo yawe ya jumuia au jamii nzima?

Punguza jaziba na mapovu mkuu na maisha yatakuwa rahisi tu. Kumbuka kuwa Ndesamburo hana hatia (sio fisadi) mpaka ithibitishwe vingenevyo - au wewe unasemaje?
 
Ndio maana nimemkaribisha upya JF. Huenda alipoingia hakukaribishwa kwa hiyo anamalizia hasira za kutokaribishwa kwenye kiibodi.
 
Ndio maana nimemkaribisha upya JF. Huenda alipoingia hakukaribishwa kwa hiyo anamalizia hasira za kutokaribishwa kwenye kiibodi.

Asante sana Jasusi,

Huyu Semenya amekuwa na hasira sana hapa jamvini for a while now. Juzi alimwaga madai chungu nzima hapa kuwa vyama vya upinzani havikosolewi hapa jamvini. Ilibidi SteveD atoe shule kwa kipindi kizima (bila maswali wala pop quiz).

Labda kwa kuwa umemkaribisha sasa atatulia na kufuatilia mijadala yote ya JF kwa umakini zaidi).
 
nani anathibitisha kuwa mtu ni fisadi me najua ni Court of law kama hivyo basi hata akina Lowasa et all tuwachukulie hivyo hivyo innocent till proved guilty
 
nani anathibitisha kuwa mtu ni fisadi me najua ni Court of law kama hivyo basi hata akina Lowasa et all tuwachukulie hivyo hivyo innocent till proved guilty

Ukitaka kusema kuwa Lowassa sio fisadi, unaweza kusema hivyo mkuu. Uzuri ni kuwa utapingwa kwa hoja na sio kulazimishwa kusema vinginevyo.
 
lakini ujumbe si niliufikisha mkuu
kama tunataka kuweka upinzani uwe strong lazima tukosoe nao wanapokosea ili wanaojiita CCM wasiwe napakukimbilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…