Ndesamburo anunua helkopta za kampeni Chadema

lakini ujumbe si niliufikisha mkuu
kama tunataka kuweka upinzani uwe strong lazima tukosoe nao wanapokosea ili wanaojiita CCM wasiwe napakukimbilia

Hakuna aliyekukataza kupinga au kukosoa upinzani (btw -- wanakosolewa sana hapa). Tatizo ni pale unapolazimisha watu kuandika kile unachotaka wewe (wakati huo huo ukitoa madai ya uongo kuwa upinzani haukosolewi hapa JF).
 
Mzee Ndesa si fisadi.
Welcome to JF Semenya naona umejiunga juzi juzi tu.
sijasema kama Ndesa ni fisadi
MESEMA SIVIJUI VYANZO VYAKE YA MAPATO so siwezi sema lolote labda file lake lijitokeze
 

Nadhani ni lazima pia awe mwamanchi anaetambuliwa kikatiba kuwa ni mwananchi wa nchi siyo jitu kutoka nje sijui Iran, Pakistan anakuja kuwa mfadhili wa chama!
 
hongera sana CHADEMA!
 
kwani CHADENA ikisaidia albino ni NGO?
CCM wameshafulia wametulia hela zetu tunataka kuona vyama vya upinzani vitumie pesa kwa utaratibu mzuri.

Watumie pesa zipi na za nani? Ndesa kanunulia hela zake helkopta, sio za walipa kodi wala si za wanachama kama ccm walivyofanya. Kwa hiyo huna haki ya kumhoji. Ukiwakabidhi nchi ndio uhoji matumizi ya hela ya serikali.
 

Thanks Mkuu, watu wanakurupuka bila data.
Kwa ufafanuzi uliotoa sioni hiyo hoja ya Chadema na wachagga inatoka wapi. Au wana maana Mbowe kuwa Mwenyekiti ndio kuifanya chadema ya wachaga?
 
Wamejitahidi inaonyesha wana mipango endelevu ingewezakana wangepata nyingine kama nne hivi ili wawafike wengi huko vijijini ambao wanafikiri mwalimu Nyerere bado yuko hai na kwa hiyo imani yao chama chake cha CCM ndio mtawala halisi
 
Mzee Ndesa si fisadi.
Welcome to JF Semenya naona umejiunga juzi juzi tu.

Jasusi,
Hapa naona umechemsha. Kujiunga juzi juzi kwa Semenya kuna uhusiano gani na hoja yake? Let the guy empty his brain in the forum where we dare to talk. After all, how do you know that Mzee Ndesa is clean? How many TZ businessmen are clean?
 
Unless Mzee Ndesamburo amezinunua hizi kopta kwa uamuzi binafsi, otherwise huu utakuwa ni utumiaji mbaya wa pesa. Je baada ya uchaguzi zitauzwa au atazi-paki?

Natumaini huu uamuzi ulikuwa ni wa Mzee Ndesamburo peke yake na sio wa chama, maana kwa chama huu utakuwa ni ufujaji mkubwa wa pesa.

Huwezi kununua limo kwa ajili ya harusi ya week end moja, unless ziwe zinakuwasha.
 

Huwezi kulinganisha helikopta na limo linganisha helikopta na Fuso. Helikopta ni chombo cha kazi sio cha starehe. Kwa mantiki hiyohiyo ya kutumia helikopta wakati wa uchaguzi unaweza kuitumia kujenga chama baada ya uchaguzi. Hata hivyo kuna demand kubwa ya helikopta nchini na Ndesamburo ameliona hilo. Ni biashara nzuri na sio sahihi kusema ni utumiaji mbaya wa pesa.


.
 

Mkuu Makaayamawe sijakuelewa unamaanisha nini
Yaani pesa zake (Ndesamburo) kaamua kuzitumia tatizo liko wapi?
 

Mkuu Nyumbu,
Iwe ni Limo au Fuso, itakuwa ni biashara kichaa kuyanunua kama kazi yake ni ya siku chache tu. Ndio maana nimesema kama Ndesamburo amekinunulia chama hizo kopta baada ya kujadiliana na uongozi wa chama juu ya nini awasaidie, basi amekosea kwani hiyo pesa ingeweza kutumika vema zaidi.

Lakini kama kopta ni zake binafsi na atakiazima tu chama, basi amefanya la maana. Jinsi atakavyozitumia baada ya uchaguzi ni juu yake.
 
Mkuu Makaayamawe sijakuelewa unamaanisha nini
Yaani pesa zake (Ndesamburo) kaamua kuzitumia tatizo liko wapi?

Mkuu MwalimuZ,
Kama kopta ni zake binafsi na anakiazima tu chama, basi hiyo haina shida maana ni mali binafsi. Tatizo ni kama amekinunulia chama, wakati chama kinahitaji pesa ili kukipanua vijijini.
 
Mkuu MwalimuZ,
Kama kopta ni zake binafsi na anakiazima tu chama, basi hiyo haina shida maana ni mali binafsi. Tatizo ni kama amekinunulia chama, wakati chama kinahitaji pesa ili kukipanua vijijini.

Nakubaliana na wewe,sijui viongozi wa Chadema wanatoka sayari gani, kukua kwa chama kunategemea ufikaji ujumbe kila kona ya nchi kwa kutumia baisikeli,pikipiki na labda magari.Kuruka kwa helikopta wakati wa uchaguzi na kuwatimulia wananchi vumbi nyingi kamwe hautafanikisha kukiendeleza chama na kuwashawishi kukipigia kura.
 

Mhh, kweli?
 
.... kukua kwa chama kunategemea ufikaji ujumbe kila kona ya nchi.....

Nakubaliana na wewe hapo na hiyo ndio sababu CHADEMA inatumia helikopta. Kwanza, Watu wa vijijini wanashawishika zaidi kwa kuwasikiliza viongozi wa kitaifa sio walewale viongozi waliowazoea. Ukimpeleka kwa baiskeli au pikipiki hawatamsikiliza, watampuuza. Ndivyo Watanzania tulivyo. Lazima aende kwa gari. Helikopta inafika kwa urahisi zaidi na inafika sehemu ambazo gari haifiki. Pili, Kwenye kijiji cha watu elfu moja ukienda na baiskeli, pikipiki au gari hata utangaze mkutano namna gani hutapata watu zaidi ya mia lakini ukienda na helikopta unapata zaidi ya watu mia tisa. Wataishangaa helikopta kwa dakika kumi halafu wataanza kujiuliza huyo aliyekuja nayo ni nani na anatafuta nini? Watakusikiliza. Kwa wiki mbili zijazo kijiji kizima kitakuwa kinaongelea ujio wako tu! Ukicheza karata zako vizuri Ujumbe unafika KISAWASAWA.

.
 
Wamefanya vizuri sana kwa ajili ya hilo maana kuna ulazima sana katika kujua mambo na kujitayarisha kwa ajili ya mwakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…