Ndevu na Vinyweleo kwa Wanawake husababishwa na Nini...????

Amanijua

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
1,776
Reaction score
1,619
Nimekua nikijiuliza sana hili swali bila kupata majibu yenye mashiko...

Na Leo asubuhi nikiwa napita kwenye jengo la CCM makao makuu nimekutana na mdada ambaye kwa kumwangalia anaweza akawa kwenye late 20's. Lakini kidevu chake kimejaa ndevu na inaonyesha hajawahi kunyoa.

Hali hiyo ipo hadi miguuni na eneo la kifuani.

Sasa kwa wale wenye ufahamu na hili naomba wanipe elimu ili kama kuna precautions ambazo wazazi watarajiwa wanaweza kuzichukua pale wanapokua wajawazito ijulikane,maana nilishawahi kumsikia mzee mmoja akisema mwanamke mjamzito akiwa anapenda sana aina Fulani za vyakula hupelekea kupunguza feminine hormones endapo atakua amebeba ujauzito wenye mtoto wa kike.....
 
Amanijua kwa knowledge chache biliyonayo mimi huyu dada anasumbuliwa na tatizo la kutokubalnce kwa hormones za kike na kiume,namaanisha hormones za kiume zipo juu kuliko za kike.....
Kuna ugonjwa unaitwa Polisystic ovarian sydrome(anakua na kama vivimbe vidogogodo kwenye ovaries) ambapo dalili zake ndo kama ndevu,nywele za kichwani kuwa nyepesi na kukatika au hata kipara,siku za hedhi kuwa hazina mpangilio,kunenepa haraka haraka........
 
Last edited by a moderator:
mwalimu wangu wa history alizoea kusema 'the more hair you have the more primitive you are'
 
Du mkuu dalili ulizosema mm ninazo kwa hiyo mm naumwa huo ugonjwa
 
Hizo ni hormones mkuu zikizidi ndio hivo tena, hadi wanaume wapo wana makota na hipsi za ukweli
 

Mkuu Mimi Nina ndevu na vinyweleo vingi ila hizo dalili nyingine sina kabsaa...kwahiyo ntakuwa na huo ugonjwa au????
 
Last edited by a moderator:
Hizo ni hormones mkuu zikizidi ndio hivo tena, hadi wanaume wapo wana makota na hipsi za ukweli

Mmmmmmhhh hiyo nayo Kali mkuu ila nasikia kuna precautions ambazo wajawazito wanaweza kuzichukua ili kupunguza hiyo possibility....
 
Ebu tuambie mkuu kama umewahi kuzinyoa maana wengine eti wanaogopa kwenda saluni kunyoa wakiwa na hofu ya kukua zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…