R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
MAHAKAMA Kuu ya Vuga, mjini Zanzibar, imetoa ushauri kwa viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislamu Zanzibar, wanaotuhumiwa kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa Taifa, wanaodai kutotendewa haki wakiwa gerezani, wafungue kesi ya madai.
Hatua hiyo, imekuja wiki chache baada ya viongozi hao kunyolewa ndevu wakiwa mahabusu (Chuo cha Mafunzo).
Ushauri huo umetolewa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi, baada ya kupitia kwa makini maombi ya watuhumiwa hao yaliyofikishwa mbele yake Novemba 8, mwaka huu, kupitia kwa mawakili wa watuhumiwa.
Kesi hiyo inawakabili watu wanane, akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikhe Mselem Ali Mselem.
Wengine katika kesi hiyo, ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.
Akitoa uwamuzi huo, Kazi alisema watuhumiwa wana haki ya kufungua kesi Mahakama Kuu kwa kile wanachokilalamikia, kunyolewa ndevu.
Kwa kupitia kwa mawakili wao, watuhumiwa hao walidai kuwa wananyimwa uhuru na haki zao za msingi, ikiwamo kupigwa marufuku kufuga ndevu wakiwa rumande, maarufu kama Chuo cha Mafunzo (Magereza).
Watuhumiwa hao, wanakabiliwa na makosa manne, yakiwamo ya kutoa lugha za uchochezi, kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara mjini Zanzibar.
Wakizungumzia kesi ya msingi kwa watuhumiwa hao, waendesha mashtaka wa Serikali, walidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamili na kwamba wanaomba siku nyingine ya kutajwa.
Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 29, mwaka huu, itakapotajwa tena.
Kama kawaida, Jeshi la Polisi lilifunga barabara zote za kuingia na kutoka mahakamani na kuimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama hiyo, ambapo kila pembe walionekana makachero wa polisi na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Nao baadhi ya wananchi waliofika mahakamani hapo, waliwataka waandishi wa habari kuandika ukweli kuhusiana na kesi hiyo ili kuinusuru nchi kukumbwa na machafuko.
Watuhumiwa hao, wanatetewa na Mawakili wa kujitegemea, Salum Toufik na Abdallah Juma Kaka, huku upande wa Serikali, ukiwakilishwa na Ramadhani Nassibu na wenzake wawili.