Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,715
Kwenye elimu yupo pia Jah People kule Njombe na yeye siku zote amekuwa akijisifu ni darasa la saba tena lile la juu. Lakini kwenye Ujambazi nadhani unahitajika uthibitisho ni tuhuma nzito saana hizo!Huyu sijui TAKUKURU wamemkosaje? Alikuwa anatoa rushwa waziwazi.
Shughuli zake hazieleweki vizuri na kuna malalamiko mengi dhidi yake toka kwa wananchi juu ya Ujambazi.
Hivi Millenium hii ya pili bado viongozi wasio na Elimu wala maadili wana nafasi???
CCM safisheni aibu kama hizi!! Wapiga kura tunaona na tutaamua
hongereni kwa kumtoa selelii.... pia hoja yenu ya uraia imewasaidia sana, well donenadhani kwa elimu ya msingi RUKWA wameongooza ...sina tatizo nao anyway ingawa kwa karne hii?????anyway anyway
nadhani kwenye hii list kuna wauza madawa ya kulevya (madai sina uthibitisho), mafisadii, walaghai, wazinzi (wanaoambukiza watu VVU kwa makusudi -madai tu sina uthibitisho) na waporaji...yote haya ni sawa tu au ujambazi ni extreme case???
mix with yours
acid unanipa hongera mimi.....kulikoni?hongereni kwa kumtoa selelii.... pia hoja yenu ya uraia imewasaidia sana, well done
hongereni kwa kumtoa selelii.... pia hoja yenu ya uraia imewasaidia sana, well done
Nchi imeangamizwa na wasomi, nikianzia na Dr Balali, Dr Andrew,Chenge, Dr Kikwete, Prof Kapuya, Dr Kamala, Dr Nchimbi wale wanasheria wa IMMA nadhani wananchi wanajaribu turufu na wale wasio na elimu! Tanzania bila elimu inawezekana. Nimewapenda hawa kuwa kweli kuliko yule Chitalilo, Dr Mzindakaya, Dr Nagu, Dr Mathayo David
Kwa hiyo itakombolewa na wa darasa la saba?
KWA WALIOPO CHADEMA..........MUULIZENI WAZIRI WA ZAMANI ALIYESHINDWA NA HUYU BWANA ATAWAAMBIA YOTE(kuhusu ujambazi na utekaji akishirikiana na wakimbizi).........! ILA HAITAKUWA GIA YA KUMSHINDA KWANI CCM HUKU HAINA MPINZANI......!
Kwa hiyo itakombolewa na wa darasa la saba?
Mkuu hujanisoma wasomi wetu wanasiasa hawana tofauti na darasa la saba waliowengi! Richmond haikusainiwa na Ngumbalu, Deep green hawakuwa darasa la nne! Mikataba ya kilezi ya madini ni wasomi wetu! wala rushwa na drugs dealers ni wasomi
common hebu waacheni hao wakweli wa elimu ndogo wafanye mambo afterall ubunge hausomewi
complitilyi non senseVibaraka wa mafisadi mnajitokeza mmoja mmoja bila kujijua!! Mmefulia ile mbaya; njaa itawaua!!
Huyu sijui TAKUKURU wamemkosaje? Alikuwa anatoa rushwa waziwazi.
Shughuli zake hazieleweki vizuri na kuna malalamiko mengi dhidi yake toka kwa wananchi juu ya Ujambazi.
Hivi Millenium hii ya pili bado viongozi wasio na Elimu wala maadili wana nafasi???
CCM safisheni aibu kama hizi!! Wapiga kura tunaona na tutaamua
CCM yapitisha aliyetajwa kuuza viungo vya Albino
Mwandishi WetuAgosti 18, 2010
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) iliyokutana Dodoma kuchuja na kupitisha majina ya wagombea wake wa ubunge, imepitisha jina la mgombea ubunge aliyewahi kupigiwa kura na wanakijiji akitajwa ni muuaji na mnunuzi wa viungo vya maalbino, Raia Mwema imebaini.
Mgombea huyo (jina linahifadhiwa) ambaye sasa atakuwa ameweka rekodi ya kushinda kura ya maoni CCM pamoja na kura ya maoni ya mauaji ya maalbino iliyowahi kuendeshwa na Serikali, ni kutoka katika jimbo moja (jina linahifadhiwa) mkoani Kigoma.
Gazeti hili limefanya uchunguzi na kuwasiliana na vyombo vya usalama, na kuthibitishiwa na baadhi ya wakazi jimboni humo ambako mgombea husika ameteuliwa kugombea ubunge. Taarifa tulizo nazo zinaelekea kumshutumu mteule huyo wa CCM kwa makosa kadhaa ya jinai, na mshangao ni wa jumla kuhusu uteuzi wa mtu anayeonekana hafai kwa kigezo chochote isipokuwa matumizi ya fedha na ufadhili wake kwa wakuu wa chama.