NDIKI, ni kitendo, pale ambapo watoto mnataka kucheza mpira

NDIKI, ni kitendo, pale ambapo watoto mnataka kucheza mpira

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
*NDIKI*
Kwa wale waliozaliwa Dar es Salaam haswa miaka ya sitini na mwanzoni mwa miaka ya sabini wanalijua neno hili NDIKI.

NDIKI, ni kitendo, pale ambapo watoto mnataka kucheza mpira, inabidi timu mbili ziundwe miongoni mwa watoto walioko uwanjani, sasa kinachofanyika, wote mnakaa mstari mmoja katikati ya uwanja, halafu wanatokea wachezaji wawili ambao ni bora miongoni mwenu na kukaa pande mbili tofauti, baadae wachezaji hawa kwa kupokezana kila mmoja anamtaja mchezaji anae mtaka aende upande wake. Mara nyingi awamu za kuchagua ziko tatu au nne. Inategemea kama mpira ni wa wote au kuna mtu mwenye mpira wake..

Awamu ya kwanza wanaaza kwa kuchagua magolikipa,
Awamu ya pili atachaguliwa mwenye Mpira, hata kama hajui kucheza, na wakati mwengine yeye anaweza kuwa mmoja wa wachaguaji hata kama yeye siyo bora, awamu hii inaweza isiwepo kama mpira ni wa wote.

Awamu ya tatu, kwa kupokezana, kila mtu anaita jina la mchezaji amtakae, hapa wataanza kuchaguliwa walio bora Zaidi, hadi waishe.

Awamu ya nne ni ya wale makapi (Bahati nzuri mimi sikuwa kwenye hili kundi), wale ambao wanatakiwa kujaza idadi, lakini hawajui kucheza, na wakati mwengine ni bora kutokuwa nao kwenye timu sababu hawajui na wanaweza kufungisha, awamu hii wale wachaguaji hawachagui tena bali wanalazimishana mtu aende upate wa pili, utasikia “Fulani mchukue wewe mimi tunatosha” kipindi hiki hawa jamaa huwa wanatia huruma wakati mwengine hukosa upande wa kucheza na kuishai kuokota mipira ikitoka.

MIMI BINAFSI, ALHAMDILLILAH, NILIKUWA NAGOMBEWA KUPITA MAELEZO, MAANA KABUMBU NILIKUWA MTAALAMU.

*SASA KIPINDI HIKI CHA NDIKI YA SIASA AMBACHO WANASIASA WANA HAMA TOKA CCM AMA UKAWA NA KWENDA UPANDE WA PILI SIJI NI AWAMU YA NGAPI KWENYNDIKI
 
Mimi nilikuwa mchezaji mzuri kwa hiyo nilikuwa nalinga hata mwenye Mpira akinichagua kwenye timu ambayo siitaki nilikuwa naondoka
 
Pia kuna walio wahi kuwa wanawashikia no magwiji Pengine kachelewa bado anapasua kuni....Hapo akija basi anatolewa MTU yy aingie
 
Back
Top Bottom