Ndimu ya Mchange: kufurahia tozo kufutwa ni kufurahia umasikini

Wizi tu tozo ni wizi mkubwa kwa wananchi,siku jua likichomoza na nuru kupatikana tutawashtaki wakiwa hai au wamekufa.tutawashtaki kwa mengi wanayofanya.
 
Huyu Machangeni nani ? asitutishe kwanza hamna aliyekataa Tozo, bali ni kiasi gani cha Tozo na kikatwe kwenye miamala gani sio kila mwamala ukatwe tu kisa tunataka maendeleo......shubaamit.
 
Wewe kama unakubali si upeleke hela zako wakanunulie V8? Mtu mwenyewe kula kulala Mchange unatupangia kipi cha kupinga, kipi cha kusapoti?
 
Serikali makini huwa inafanya adjustment kwenye matumizi yake ili kuendana na Hali halisi ya maisha hapa kwetu ndo kwanza wanatapanya pesa
 
Mkuu mchange, pole kwa msiba pale kawe.
 
Habibu Mchange ni punguani! Hapo anavizi uteyuzi siyo kwa kujitoa ufahamu hivyo! Yaani tutozwe watu waende wakafuje hela yetu? Wameshindwa nini kusimamia raslimali tulizojaliawa wakawekeza kwenye huduma za jamii?
 
Tumeendelea na kutozwa tozo, na kuombaomba ndo imeongezeka Mara dufu!

Wewe Change huoni hili?

Hizi tozo tunazotozwa bila kupewa listi ya Serikali au ya TRA, tunajuaje sisi ikiwa ni kweli zinaingia serikalini au zinaishia Kwa wajanja?

Mbona hamzitangazi kama ilivyokuwa awali?

Haieleweki zinajenga nini hizo tozo, madarasa ni zile za Kovidi, Sjui madarasa ni za mkopo Kutoka wapi huki, hizi za tozo ni sh ngapi na zinaenda wapi?
 
Tozo haina maana yoyote,Ibakie kodi tu.
Serikali ipunguze matumizi kukabiliana na hali ngumu
 
Anza kulaumu serikali ya awamu ya tano kwa kuuwa miradi ya watu kupora pesa za watu mabenki na kukimbiza wawekezaji kwanza. Makufuli alijua anajenga kumbe wamejimwagia petroli. Wasingegusa maisha ya watu angalau watu wangevumilia.

Tupe kwanza mchakato wa hayo magari ya msafara ya milion 500 kuanzia ofisi ya rais Hadi kwa mkuu wa wilaya na wizara yanapatikana vipi ndio tuendelee na mjadala.


Unakwenda kuzindua zahanati ya milion 50 unakwenda na msafara wa mabilion ya pesa.

Halafu unasema unahitaji mchango wa tozo.

Huyu mdudu tozo akafie mbali.
 
Kabla ya tozo hali ilikuwaje? Mbona hata baada ya tozo madeni na kukopa vimeongezeka?
Hawa wajamaa inaonyesha hayo magari ya misafara wamekopa. Sasa ngoma ya kulipa wakiondoa tozo itakula kwao.

Watuambie Hapo ndani ya tozo Pana ulazima gani kama wananchi hawataki?

Kwa Nini tunalazimishana, badala ya kutafuta mbinu za ajira kwa vijana wetu wanasumbua raia na tozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…