Mpauko
R.I.P
- Jan 19, 2019
- 2,323
- 3,428
Nilikuwa mahali nakula na kufurahia msosi na coca yangu bariidiii, mara akaingia mwanaume kabeba briefcase.
Kwa mwonekano lazima ni mwanasiasa mkubwa au bosi mkubwa mahali maana uvaaji na mwonekano wake ikiwemo kitambi chenye ujazo wa afya vilithibitisha taswira yake.
Aliingia kwa madaha na kila mmoja hotelini alivutiwa nae na tulimsindikiza kwa macho hadi alipoketi,Mara kuna mwanamke akamfuata akiwa analia kwa uchungu akapiga magoti mbele yake na kumueleza kuwa wanae na mama yake mzazi wako katika hali mbaya ya kusubiri kifo kwani hana chakula kabisa nyumbani na mumewe alishafariki.
Bosi kwa huruma akafungua briefcase na kumpatia yule mama shilingi milioni tano taslimu,Yule mama aliruka kwa furaha kumtukuza Mungu na kumshukuru bosi yule.
Mara tena akaingia kijana mwenye bahasha mkononi mara alipomuona yule bosi akashuka chini magotini kwa tajiri na kuanza kulia akiomba amsaidie mtaji aanzishe biashara kwani pamoja na kusoma hadi chuo kikuu amekosa pa kuajiriwa.
Hivyo bosi akatoa kitabu cha hundi na kumuandikia yule kijana hundi ya milioni 10 akampatia yule kijana.
sasa uzalendo ukanishinda wa kuangalia wenzangu wanapewa hela kiulaini, Nikaanza na kujibubujisha machozi huku nikiendelea kuhesabu shida zangu ili nami nipate dau kubwa toka kwa bosi msamaria.
Nikamsogelea yule bosi huku nalia nikapiga magoti chini mbele yake, mara nikasikia sauti kavu na kali ikisema:
Cut!!
Cut!!
Cut!!
Nikageuka na kukutana na mwongoza filamu, akaniambia, ..........ondoka hapo sie tunarekodi filamu.
Alaa...kumbe haya ni maigizo! Ni nani ana moyo kama huo,hayupo,haiwezekani!...nikaondoka zangu.!