Ndio tuseme Mbowe kapoteza nafasi adhimu nyingine?

Ni kwamba wewe humjui Mbowe na asili yake. Umeokoteza vijimaneno vya hapo Lumumba na vijiwe vyenu na kutengeneza story kututoa kwenye agenda muhimu.
Unaonekana kama mtu timamu wa akili lakini sio ajabu wenye akili wakakuita mpumbaf, na ikitokea basi usikasirike bali jitafakari.
 
Hivi Mbowe anakwenda huko kwa agenda ya wananchi au agenda zake mwenyewe?
The Boss,sikuhizi una tatizo gani kwenye ujengaji wa hoja? Kuna uelekeo flani ya kufifia kwa hoja zenye mashiko kutoka kwako tangia suala la DPW ianze.
Kuna mawili, wewe ni mnufaika wa posho za DPW au unategemea kupata posho kutokana na mkataba wa DPW.
 
Tukiweka urafiki wa vyama kwenye siasa Taifa letu haliwezi kuendelea. Huo unakua ni uhuni, ni sawa na goal keeper kubet timu yake ifungwe. Kama alikua anafanya urafiki na viongozi wa chama kingine alikua anakosea.
Brother unailazimisha akili yako kuandika vitu visivyo sawa. Unapindisha makusudi.
 
Siasa ni mchezo wa Upepo na Mazingira.Kwaiyo Rais kumwita Mbowe ni kwasababu ya ushawishi na nguvu ya chama chake Wala siyo mapenzi ya serikali na CCM.
Ata Mwalimu Nyerere hakupenda kuachia madaraka mwaka 1985 ila Mazingira ya kisiasa yalibadilika kutokana na Dola la Russia kuanguka ambako ndiko support ya ideologies zake ilipokuwa.
 
Mbowe anajitahidi mno kuendesha gari isiyo na matairi. Umma wa watanzania ni vigumu sana kuhamasika kisiasa. Ni watu waoga wasiojua walitakalo. Siku CCM ikitoka madarakani hutaona mtu yeyote kule. Watanzania hupenda timu inayoshinda na hivyo hubadilisha timu kila wakati.
 
Zitto alikubali hizo "golden opportunity" zote, amefikia wapi?

Katika makosa ambayo hata mimi naona CDM walifanya ni kuachana na Katiba mpya 2014... tulirudi nyuma miaka 60.
Lile bila shaka ni kosa la kujutia sana
 
Mbowe angekua mlaini kama ambavyo hua mnataka watu waamini hivyo sidhani kama angekua hivyo leo.


Mbatia, Lipumba, Mrema na Zitto wapo wapi ukilinganisha na Mbowe?
 
Ni lini Bob alishinda uchaguzi ila akaambiwa amuachie Mbowe.Kitu haujui Bob Makani alikuwa mwenyekiti hadi alipoamua kustaafu mwenyewe. Halafu ujue Bob Makani mke wake wa pili ni mdogo wa Edwin Mtei.
 
Umeandika uongo wa bahati mbaya... yaani toka suala la bandari lianze umekuwa ukifikiri kwa kutumia matako
 
Bandiko refuu ila huna proof yani ulivyoandika hapa kama vile upo vichwani mwao...Propaganda za kijinga.
 
Mlitaka awaunge mkono kwenye utapeli na udalali wenu wa bandari baada ya kutofanya hivyo mmeanza kuwa waandishi nguli zaidi ya Shaaban Robert. Mwambieni bibi yenu aachane na bandari zetu akauze za mchambawima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…