Mdau Lunyungu! Kwa mahesabu ya Hosea nadhani hapo hujakosea kitu, suala la Karamagi nadhani DPP amerudisha jalada kwa kuwa cha kumshitaki jamaa 'hakionekani'. Kwa sasa waliobaki nadhani ndo wale Pinda anaosema nchi itatikisika na nadhani ni zamu ya Lowasa (kumbuka huyu anaheshima ya uwaziri mkuu).
Kwangu mimi nchi isitikisike kwa kumpeleka mahakamani huyu jamaa na hapo ndo tutaweza kuona mapungufu makubwa yaliyokatika katiba yetu
KATIBA BORA NI ILE INAYOTENGENEZWA KWA MANUFAA YA UMMA