Ndiyo nimetapeliwa au?

Sir Good

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2013
Posts
1,031
Reaction score
412
Heshima kwenu wakuu! Kutokana na ugumu wa maisha niliamua kujinyima nikahifadhi visent vyangu kwenye kibubu lengo lengo nifikishe japo 2ml ili ninunue pikipik na niifanye bodaboda niepukane na adha ya kutumwa.

Bahati mbaya kabla lengo halijatimia, kibarua kikaota nyasi. Kuchungulia kibubu nikajikuta nina million moja na laki moja pesa ambayo siwezi pata pikipiki mpya.

Nikamweleza rafiki yangu mmoja akaniambia kuna kampuni mpya ya kihindi ambayo inauza na pia inakopesha pikipiki aina ya Hero hivyo kama nahitaji naweza kwenda huko.

Nikaenda, kufika mapokezi nikaeleza shida yangu, yule jamaa akaniambia ni kweli kampuni ilikuwa inakopesha ila wamesitisha kutokana na ukorofi wa watu kutopeleka pesa kwa wakati hivyo kazi hiyo ya kukopesha wameikabidhi kampuni nyingine.

Akaniuliza niwapigie simu? ila wao kama kampuni wanauza pikipiki shilingi million moja na laki saba na hamsini ila kwa mkopo kupitia hiyo kampuni waliyoikabidhi nitalipa shilling million mbili na laki mbili, nikamjibu sawa wapigie.

Baada ya maongezi ya muda mfupi yule jamaa akasema "fresh nipe laki saba nikuandikie risit" nikampa, akanikabidhi risit ya kampuni inayoagiza na kuuza pikipiki hapa Tanzania na namba ya simu ya mhusika wa hiyo kampuni inayokopesha hizo pikipik, akampigia tena simu nami pia nikampigia na akaniahidi ndani ya wiki moja nitakuwa tayari nimepata pikipik.

Kweli bwana ilipofika siku jamaa akanipigia simu ili niende nikachukue, nikaenda kampuni ipo barabara ya Nyerere inatizamana kiwanda cha viatu. Kufika pale nikakutana na watu wengine, nakumbuka zilitoka kama pikipik saba hivi.

Nikampa laki 3 akaniandikia risiti. Nimepiga kazi Mungu amenijaalia nimemaliza deni kama miezi 3 hivi iliyopita baada ya kumaliza deni akaniambia nimpatie tin number ili anifanyie mpango wa kadi itayoendana na jina langu kwani hapo mwanzo alinipa kopi yenye jina LA kampuni.

Alinihaidi baada ya mud a mfupi ningeipata kadi lkn sasa miezi inakatika bado sijaipata, nimekuwa nampigia simu kaniongopea weee mpka sasa hana cha kuongopa hivyo ukimpigia simu hapokei, ukibadilisha namba anapokea ukijitamblisha anakupiga sound tu.

Nashindwa hata kubadili namba sababu sina kadi orijino, kuna mtu alitaka kuinunua kwa pesa nzuri tu lakini linapokuja swala la kadi ametoka nduki.

Mbaya zaidi nasikia pikipiki zote zilizotoka kwa njia mkopo zinakamatwa na kampuni inayoziagiza, sasa sijui tatizo liko wapi, mi nimeamua kuifungia ndani tu. Ni hayo tu wakuu ila mnisamehe kwa kuwachosha na maelezo marefu.
 
Unajua kituo cha polisi?

Kawaeleze story yote utasaidiwa.
 
Hakuenda kulipa Deni ndo maana yake! Nenda kwa hiyo kampuni na vielelezo vyako kajieleze


 
Kwa kweli umenichosha ila nimekusamehe! Sasa Mkuu kwa nini ukae unapiga simu? Kwa nini usiende mguu kwa mguu? Maana inavyoonesha na Wewe uko hapo hapo tu Dar! Je, umeshawaeleza wakubwa wake Wa kazi wanasemaje? Maana kama umeshamaliza kulipa deni kwa nini akae na kadi yako? Nenda polisi ukaeleze hilo tatizo watakusaidia! Sasa unafungia PIKIPIKI ndani ni pambo hilo? Mkomalie Mkuu tena acha kuchekacheka na huyo mpuuzi, uwe mkali kabisa!!
 
Kwa nini uishie kupiga simu tu?

Wakati unamkabidhi hela za malipo ya kadi mliandikishiana?

Kwa nini usitafute msaada wa polisi?
 
Mfuate ofisini kwake ukiwa na polisi
 
Acha uoga ingekuwa kutapeliwa ungeshatapeliwa pesa lakini siyo kadi. ungeweka wazi ni kampuni gani kama ni SABA GENERAL usiwe na wasi wasi kadi yako utapewa hu. labda kama ni kampuni ingine hao sina uzoefu nao.
 
Hakuenda kulipa Deni ndo maana yake! Nenda kwa hiyo kampuni na vielelezo vyako kajieleze

mkuu ushauri wako nimeufanyia kazi, nimeenda na vielelezo vyote yaani risiti za malipo, wakaangalia kwenye rekodi zao wakagundua jamaa amelipa laki sita tu hivyo kuna la shilling milioni moja analodaiwa na kampuni ndiyo maana wamezuia kadi. Kesho naelekea kwake vyovyote iwavyo atanitambua anipe kadi au anirudishie Pesa zangu nimpe pikipiki yake.
 

ahsante mkuu kwa kunisamehe nimekwenda Leo kumbe alikuwa alikuwa hapeleki Pesa za marejesho kampuni wanadai shilling milioni moja, kesho namfuata nikiwa na mambo mawili anipe kadi au anirudishie Pesa zangu. Kampuni imeniambia huyo jamaa ndiyo zake, kuna watu kibao amewafanyia hivyo.
 
Kwa nini uishie kupiga simu tu?

Wakati unamkabidhi hela za malipo ya kadi mliandikishiana?

Kwa nini usitafute msaada wa polisi?

risit zote za malipo ninazo
 
Acha uoga ingekuwa kutapeliwa ungeshatapeliwa pesa lakini siyo kadi. ungeweka wazi ni kampuni gani kama ni SABA GENERAL usiwe na wasi wasi kadi yako utapewa hu. labda kama ni kampuni ingine hao sina uzoefu nao.

kampuni inayoagiza hizo pikipik inaitwa Astarc Motors Tanzania Ltd, kadi wameizuia wao kwani jamaa amelipa laki sita tu.
 
Sasa mkuu watakurudishiaje pesa wakati pikipiki ulishaichakaza? Dai tu kadi yako wakupe, kwani alikuwa hakupatii risiti za ununuzi wa pikipiki ulivyokuwa unapeleka huo mkopo? Komalia kadi yako labda kama mliandikishiana mkataba ndo unaweza kufanya hivyo, na hapo itakubidi uanzishe kesi mahakamani! Vinginevyo dai kadi yako tu uendelee na biashara yako!!
 

Hatujaandikishiana mkataba mkuu,ila kanivuruga sana akili yangu kwani pikipik imekaa tu nashindwa kufanya kazi. Ahsante mkuu kwa ushauri wako mzuri.
 
Sasa pia kuwa makini asije kuprintia card fake maana zipo, mi nashauri wasiliana na hiyo kampuni anza kulipa deni taratibu mwenyewe ili uwe na uhakika na kibarua chako wakati ukiendelea kumbana huyo alipe hela zako ......


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…