Ndiyo tuna Timu nzuri, ina Morali na Mazingira yote mazuri ila nawatahadharisha wana Simba SC Mechi ya leo si rahisi kihivyo Kwetu kama tuwazavyo!

Ndiyo tuna Timu nzuri, ina Morali na Mazingira yote mazuri ila nawatahadharisha wana Simba SC Mechi ya leo si rahisi kihivyo Kwetu kama tuwazavyo!

Mzukulu

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2020
Posts
1,401
Reaction score
2,641
Kama kuna Mechi ambazo zinaenda kuwa ngumu kwa Simba Sports Club ( ambayo hata Mimi Mzukulu ) naipenda na Kuishabikia basi ni hizi Kumi ( 10 ) zilizobaki na hasa hasa hii ya Leo na zile zingine Tatu ( 3 ) ambazo zote tutazicheza katika Uwanja wa Uhuru au pale kwa Mkapa.

Sina Shaka na Timu yangu na Maandalizi yake ila tokea Juzi Moyo wangu unakuwa mzito sana hasa kwa hii Mechi ya Leo dhidi ya Ruvu Shooting. Tukishinda basi itakuwa ni Furaha Kwangu na naamini hadi kwa wana Simba SC wote ila sijui ni kwanini kuna Hisia inaniambia Mchezo unaweza kuwa mgumu sana kwa Simba SC na hatimaye ikatoka Suluhu au Sare na hata Kufungwa kabisa.

Tupigeni mno Dua ila Mzukulu nina wasiwasi na Mchezo wetu huu wa Leo kwani umetukalia vibaya na hata Kinyota si Salama Kwetu.
 
Acha woga, tutashinda mechi ya leo ingawa ni kwa magoli machache.
 
Hatimaye mliambulia droo.!

Na Mimi mapema tu kabla ya huo Mchezo nilitabiri nini hapa hapa katika huu huu Uzi wangu? Je, hakijatokea? Yanga Kesho nae awe makini Dom.
 
Na Mimi mapema tu kabla ya huo Mchezo nilitabiri nini hapa hapa katika huu huu Uzi wangu? Je, hakijatokea? Yanga Kesho nae awe makini Dom.
Kesho tunachukua point 3, hofu kubwa tuliyonayo ni jumapili dhidi ya Azam, hawa JKT Tanzania tutakomaa nao
 
Kesho tunachukua point 3, hofu kubwa tuliyonayo ni jumapili dhidi ya Azam, hawa JKT Tanzania tutakomaa nao

Ninaendelea Kusisitiza tena hapa kama nilivyokuwa na Hofu kwa Simba juzi ndiyo ninayo pia kwa Yanga Kesho. Ingieni na Tahadhari zote Ndugu.
 
Back
Top Bottom