Ndoa fasta chanzo cha migogoro mingi ya kifamilia

Ndoa fasta chanzo cha migogoro mingi ya kifamilia

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Ndoa Fasta

Ni ndoa ambazo Me na Ke wakutana bila kujuana vizuri na wakaamua kufunga ndoa.

Sasa mara baada ya kufunga ndoa ndio huanza kufahamiana vizuri kumbe mume wangu ana tabia hizi au kumbe mke wangu ana tabia hizi.

Wakishindwa kuvumiliana basi migogoro inaanza.

Migogoro ya muda mrefu kiasi kwamba watoto wanaathirika kisaikoloji, kazini mambo hayaendi amani hakuna.

Ndoa Fasta zimeleta maafa

Ndoa Fasta zimetengeneza Single mother wa kutosha.

Watoto wanateseka mara wako huku mara huku.

Watu wengi wanahadaiwa na Pesa, umbo, Magari, Nyumba, Biashara bila kuangalia tabia za mhusika unaeenda nae kufunga nae pingu za maisha.

Turudi kwenye misingi ya kusikiliza ushauri kutoka kwa wazazi. Lakini pia kufuatilia kwa kina taarifa za mtu unaetaka kufunga nae ndoa.

Wengine wamefunga ndoa na wame au wake za watu baadae ndio wanakuja kujua.

Kwenye masuala ya Mirathi inaanza kuwa tatizo na watoto wanapoteza haki zao za Msingi.

Turudi kwenye misingi Jamani tusitamani ndoa za Instagram au mitandaoni kwa ujumla.
 
Vijana mkifikia umri wa kuoa washirikisheni wazazi hasa wakike wanawake wanajuana jifanye mjuaji ukutane na pornstar
Mwisho wa kunukuu.
 
Back
Top Bottom