Katika siku hizi za karibuni tumeiona nchi yetu ikitumbukia katika matatizo makubwa ya ufisadi wa kutisha,pamoja na ukweli kwamba uovu mwingine pia umeongezeka katika kiwango cha kutisha.Lakini kwa maoni yangu mimi,uhusiano huu ambao sio sahihi kati ya CCM na Serikali, umetuingiza katika matatizo makubwa sana.Tumeshuhudi fedha za wavuja jasho zikichotwa na kupelekwa kwenye uchaguzi.Hatujui kwa uhakika ni kiasi gani,lakini ninaamini zilizochotwa kupitia EPA sio picha halisi.Hatujui kwa uhakika za Richmond,EPTL nk.ziliishia wapi,inawezekana CCM.Ninachojiuliza siku zote ni kwamba hivi CCM haina ubunifu wa kutosha wa kujipatia fedha zake yenyewe mpaka iwaibie wananchi,ambao kwa bahati,mbaya inatamba kwamba inawatetea?Hivi CCM itaomba majamvi msibani mpaka lini?Wananchi hao hao inaosema inawatetea inazidi kuwafukarisha kupitia kwenye mgongo wa serikali.Kikwete amka bwanaaa.