Ndoa imenishinda...Your Advice PLS!

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412
Jemeni sasa huu mwaka mmoja na miezi 2 sasa nimo katika ndoa lakini mambo ninayokumbana nayo kwa kweli ni makubwa mno, yamenielemea. Nimeona bora nimwage mtama hapa jamvini ili wenye nia njema wanipe ushauri wa kufanya. Mwaka jana mwanzoni nilimuoa binti wa Kitanga anatoka Pangani.Siwezi kueleza yote lakini huyu mwanamke ana matarahambe sijapata kuona, kila nikijitahidi kumridhisha hatosheki, tukianza kugombana basi anapiga kelele mpaka majirani wote wanasikia, aibu tupu!! Kwa mfano mara nyingi yeye anapenda nimnunulie nyama ya kuku, Juzi nilipita Kisutu nikachukua kuku 4, kufika nao nyumbani, ananiambi eti kachoka kula nyama ya kuku, anatamani kula nyama ya kasuku, nilishtuka sana, nikamuuliza kama yuko serious, akaniambia hivyo ndivyo anavyotaka, nimejaribu kuulizia kasuku anauzwa bei gani, nimeambiwa mmoja ni laki mbili, hivi wadau mnanipa ushauri gani?? Huyu mke si wa kuachana naye!! Au kuna njia yoyote ya kufanya....
 
Aithee kumbe umewowa mkuu duh kuhusu kumuacha sina la kuongeza kwani uamuzi wa kuoa ulikuwa ni wako, na kuacha kwa nini usiamue mwenyewe tu
 
hujamuelewa, anakupenda sana huyo............endelea kumstudy, kuna ka-kitu hujamjulia..................... watu kama hao anamatch vizuri zaidi na "vijana"..........nadhani unanipata kiutu-uzima................. i mean punguza "heshima" unayompa, ongeza "matusi" (rejea enzi za bi chau na mzee small) kidogo, ongeza na "uchokozi"................mtafakarivizuri huyo kasuku anayemtaka, unaweza hta kurejea "tanga kunani"...................etc

huyo ni mke bomba sana, usithubutu kumwacha , tena usimgeuze BWABWA. ........... analipa kishenzi huyo...................... yakikushinda kabisa, kawaangukie wazee wakufunde upya, ukianzi pangani na kumalizia kwenu..............
 
Akili kichwani hapo umenisuza roho, kumbe unazijua hata zile tamthilia za kina bichau, wewe utakuwa mtu wa mwambao, unatokea wapi ndugu yangu??
 
Akili kichwani hapo umenisuza roho, kumbe unazijua hata zile tamthilia za kina bichau, wewe utakuwa mtu wa mwambao, unatokea wapi ndugu yangu??

ndio maana ya akili ichwani mzee...................................
 
He! Ukistaajabu ya BWABWA! BWABWA Ameongoka LoL!
 
preta mpaka sasa hivi hujalala? pole sana, mimi shoga wa kinyume na maumbile, usihofu lakini...hii inatokana na maumbile ya kuzidiwa hormons nyingi za kike mwailini

Nakumbuka ulishakiri kwamba wewe ni shoga(unayeingiliwa kinyume na maumbile)...Isije ikawa ndiyo sababu ya binti kuanza kukuletea vituko aisee,maana kaona kuwa na mume BWABWA mhhhhhhhh
 
Nakumbuka ulishakiri kwamba wewe ni shoga(unayeingiliwa kinyume na maumbile)...Isije ikawa ndiyo sababu ya binti kuanza kukuletea vituko aisee,maana kaona kuwa na mume BWABWA mhhhhhhhh
Umeanza Balantanda.....
 
duh! makubwa haya kasuku analiwa pia???a first one for me....or what kasuku is this?
 
inachekesha jamani dunia ina mambo na mie nitaanza kuomba nyama ya ngamia
 
inachekesha jamani dunia ina mambo na mie nitaanza kuomba nyama ya ngamia

utaachwa shauri yako......mind you ukiachwa ndoa yangu husimamii bestilady wangu ohooooooo!!!
 
utaachwa shauri yako......mind you ukiachwa ndoa yangu husimamii bestilady wangu ohooooooo!!!

Kumbe ndo bestlady wako huyo.....Mi bestman wangu unamjua lakini??
 
Kumbe ndo bestlady wako huyo.....Mi bestman wangu unamjua lakini??
sijamjua na hivi mipango yenyewe imeanza kusuasua ngoja nifunge mdomo wangu nisije nikawa simulizi mjini
 
sijamjua na hivi mipango yenyewe imeanza kusuasua ngoja nifunge mdomo wangu nisije nikawa simulizi mjini

Heheeeeee,wala usiwe na wasi...Kila kitu kitaenda kama kilivopangwa mamii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…