ndoa inanishinda nipen mawazo yenu

Mimi huwa ni mkali kwa watu wanaoolewa na wanaume kama huyo mume wako (alokwisha hachana na wanawake kadhaa) lakini dada umenifanya niwe mdogo. Unaonekana huna makosa. Mmeo alikulaghai kwa kuwa ulikuwa mdogo na labda alikuwa (au bado) ana pesa ukadhani hayo ndio maisha. Pole sana. Ila sikushauri umwache mumeo kirahisi. Fight my dear fight for the man you love! Maana kam huna kipato utaishia kuwa mikononi mwa mapedeshee wengine wasiothamini utu wa mwanamke.
 
Bora ungesema asizae mtoto mwingine kwani future haiko certain. Dada jitahidi usishike mimba tena maana ndoa yako haieleweki isije ikawa ngumu kulea watoto baadae

 
huyu dada ameolewa na 17yrs ulimaliza hata shule kweli mamito? na una hata ujuzi wowote? umasikini kweli mbaya wazazi wako kisa cha kukuozesha mdogo vile? nakushauri rudi shule upate elimu na ujuzi ukiwa serious utatoka. umesema unafikiria kuachika kwani we bado ni mzuri so unategemea uzuri wako kuishi sio? na kama ni hivyo sioni haja ya wewe kuachika kwani ili uishi lazima uwe na mwanaume wa kukuwezesha. Naona bora ubaki tu na huyo huyo ila rudi shule
 
Bora ungesema asizae mtoto mwingine kwani future haiko certain. Dada jitahidi usishike mimba tena maana ndoa yako haieleweki isije ikawa ngumu kulea watoto baadae

nyumba kubwa nadhani hujanielewa ninachokielezea hapa..........asizae mtoto mwingine ? Kuzuia mtoto inasaidia? kunamakubwa kuliko mtoto. Kwa mume kama huyo kuna maradhi ambayo ukiyapata ni afadhali ya mimba na mtoto! na ninajaribu kuweka bayana situation ambayo wengi wetu hatuielewi either kwa kuwa haijatufika au hatujawahiiona............. tatizo langu ni juu ya mambo mawili
1. Kwa yeye kutamani nje ili awe na wa nje...sidhani kama inasaidia
2. Kumnyima mume unyumba........jamani hivi kweli hata mume akiendashtaki kuwa umemnyima unyumba utatoa ushahidi gani kuwa ni malaya??................. ulipokubali kuolewa/oa ulikuwa unasign mkataba kuwa wewe ni wa yeye na yeye ni wako so any denial of the supposedly marital rights ni violation ya mkataba wa ndoa mlousign wenyewe kwa hiyari yenu tena mkitabasamu.

My point here ni kuwa asiwe vuguvugu (eti kutoka nje ndo kumkomoa mume ) la hasha ni bora akawa baridi au moto kkwa kuamua kumwacha na kustand alone.
 
Aksante Husninyo......na kama hawezi basi aquit jumla lakini si kuiba nje,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

mi huwa nashangaa inakuwaje mtu ananyanyasika ila bado yupo tu. Duh! Sijui kama nitakuja kuwa na moyo huo wa uvumilivu kiasi hicho.
 
Mwanajamii, nimeshauri asiendelee kukutana kimwili kwavile jamani huyu mwenzetu ana mtoto na bado yeye ni kijana mdogo, mzee wake alishaoa na kuacha mara 2 na bado anafuata wanawake wadogo, ss yeye she's 23 sijui anafuata underage ?

Mimi naangalia kama ni sexual pleasure, he is already getting it from various concubines, mdada aweke akili, kwavile jamaa anafund vizuri hapo home, aombe kusoma hata nje, ukiwa shule unapanuka mawazo na kikubwa unapata skill

Nakuomba sana umwombe hela ya kukuwezesha kusoma, nje au ndani ya nchi hii marriage ilivyo chungu angalau ugain sth, kuhusu kuendelea kushiriki kimwili na mtu anayechovya kila sehemu, mm kwakweli sifagilii, niko ndani ya ndoa for abt 8yrs and am very specific ndio hayajanikuta , lakini nisingeweza kuwaweka kwenye risk wanangu 3 kwa mtu anayechojoa kila kona....

Eng
 
Hata hizi dini tunazo ziamini zinaruhusu mke au mume kuomba talaka, pale mmoja anapokwenda kinyume ba mkataba wa ndoa. Na sababu kubwa ya mke au mume kuachika ni kwa mmoja wao kuwa mzinifu au kuwa mwasherati.

Uvumilivu wako unaweza kukuletea maagamizi, kama umesha thibitisha kuwa mumeo ni Mzinifu na umemueleza lakini hataki kujirudi, basi ni bora kuondoka kwenye hiyo ndoa...!

Umri wako bado mdogo sana, Mwenyezi Mungu anaweza kukujaalia ukapata Mume aliye bora na mwenye kukupenda kwa dhati ya moyo wake kuliko huyo ambaye anajivunia pesa zake za matuzo yako na mtoto, na wakati mwingine kutoa hongo kwa wazazi wako.
 
Pole ila shida ni moja, umeolewa halafu unajiita MISS kwanini usiweke MRS?
 
Pole sana dada. wana JF wamekupa ushauri sana. Ila mimi naomba nikushauri kuwa next time ukipata hizo simu za jamaa, usihangaike kumpigia simu. Kwani ulimpigia simu kwa nini? Si unaona majibu uliyopata yamekuumiza moyo zaidi? Tumia hiyo namba ya simu kwa namna nyingine... ziko nyingi sana.
 
Katika mambo magumu kushauri ni masuala ya ndoa na ya ndani ya nyumba za watu...Uzinzi si kitu chema hasa ukizingatia madhara yake yalivyo mengi kwa wakati tulionao sasa! Kumwacha huyu bwana si suluhisho hasa ukizingatia ukweli kwamba kumwacha kwako hakutambadili mwenendo wake wa maisha!

Nadhani mna wazee/watu wazima ambao wanakusikilizeni...kaeni chini wenyewe...zungumzeni,tumia talanta yako km mwanamke,mweleze na endapo hatobadilika tumia wazee na viongozi wa dini ikibidi ili uweze kuokoa ndoa yako...Pia chunga sana malipizi,kutoka nje ya ndoa hutamkomoa huyu bwana sana sana unajiweka pabaya zaidi, na mwanenu angali mdogo anayehitaji malezi yenu!
 
njoo kwangu nora, mtoto tutalea na tutaongeza mwingine ikibidi u are too young for the experience
 
Unampotosha mwenzio
 

nashukuru na wewe kama umeliona, wengine wanamshauri atumie condom...cjui kama wanaelewa maisha halic ya humu ndani au wenzetu cjui wamebahatika kupata wenzi wa namna gani..
 

unakatisha tamaa....ina maana awote waliochana wana hiyo tabia? hiyo ni tabia ya m2 binafc, hayo mengine dada kuna kinga kwa mumeo wa ndoa kutumia kinga ni ngumu sana labda nyie mmewapata wengine condom kwa waume ze2 ni kitendawili.
 
Siteti na moyo wako ila nasema na fikra zako zisije zikazaa tabia
 

Mmmmh!!Hofu yangu hapo kwenye nyekundu isije kuletea nyekundu ...aaah!!nauhakika gani kama bado?any way nenda kafanye blood check up kama bado hujalipuka chapa lapa ya kwa Mwaisapile yenyewe bado haijathibitishwa ...mtoto mmoja nini bana naamini ukienda kutuliza kichwa wala hutashindwa kumlea huyo mtoto dada angu ila ikiwa tayari usharipuka mwambie mungu ahsante kwa ulipo fikia maisha bado yanaendelea.
 
kama wenzio waliotangulia walimshindwa huyo mwanaume na wakatoka wewe hutaweza kabisa nazungumza hivyo kwa kuwa nimeyapitia hayo, huyo mwanaume ni tabia yake hawezi kuiacha hata ungekuwa malaika cha msingi fanya uamuzi sahihi anza kutafuta namna ya kuanza maisha mapya ukiwa peke yako la sivyo tegemea kuletewa maradhi mdogo wangu, pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…