Ninamchumba sinamuda nae mrefu ninamiezi nae3 ndani ya miezi hii aliniforce ili alete barua kwe2 nikamruhusu. Nikackia kumbe alikuwa na mwanamke kampa mimba nikajamuuliza kakubali kama alikuwa nae ila kuhusu mimba ye hajui. Nikamkataza kucheza kamali kumbe bado anacheza kwa kujificha. Juzi katoka kuliwa laki 7 za kazini hakubakiwa hata sent leo nimepata fununu kutoka kwa wasichana wa karibu yake wanadai nimeingia mkenge hvyo nataka nimwambie aje achukue barua yake sitaki tena kuolewa nae. Au mnanishauri vp ndugu zangu
Angalia moyo wako unasemaje juu yake, je umejaribu kukaa nae na kuzungumza nae kuhusu mambo yake ambayo huyataki? Kama ndiyo na unaona hashahuriki chukua chako mapema mwaya usije poteza muda wako bure baadaye ukaja jutia.
Uwezo wa kumbadilisha mpenzi wako unao dada,angalia nafsi yako imeshiba vipi juu yake lakini kama unahisi haupo safe na anakuweka roho juu juu nakushauri mrudishie tu barua yake ya posa so kwa ujumla maamuzi ni yako dada.
Mpe muda, saa nyingine maneno ya kusikia ni uzushi. Fanya mikakati ya kuhakikisha, jaribu abadili tabia at the same time mambo ya ndoa kwanza yaweke on hold.