Kweli kabisa mkuu maana kuna wanaume wamewaachia mama zao waongoze nyumba zao mpaka hurumamwanaume ukiwa dhaifu hata jirani au hata hosegirl anaweza kuingilia ndoa yako.....
ukiwa strong hata nani hathubutu....trust me...
mwanaume ukiwa dhaifu hata jirani au hata hosegirl anaweza kuingilia ndoa yako.....
ukiwa strong hata nani hathubutu....trust me...
Kweli kabisa mkuu maana kuna wanaume wamewaachia mama zao waongoze nyumba zao mpaka huruma
ninapenda mwanaume mwenye msimamo kwa kweli, kuna dada angu mumewe alikuwa anaambiwa na dada
ake eti kilaukifika nyumbani tu unaenda kukaa chumbani na mkeo, na sie tunataka kuongea na wewe
yule shemeji alimjibu kama unamwona anafaidi kuongea na mimi njoo na wewe tuongee, ilikua kesi kubwa
lakini meseji ilifika wakakoma, sasa dada anaishi kwa amani
Matatizo ya ndugu au wazazi kuingilia ndoa ni suala linalotajwa sana katika kuvunjika kwa ndoa nyingi. Wengi wetu tunajua kwamba kwa mila na desturi zetu(ambazo ni potofu hata hivyo) ndoa inakuwa ni ya ndugu na wazazi pia, siyo wanandoa peke yao.
Lakini kwa bahati mbaya sana, katika ndoa nyingi, ndugu wa wanaume ndio ambao huingilia ndoa kwa kuwasakama wake katika ndoa hizo. Kwa mila na desturi hizo hizo, wanaume wengi hujikuta wakiwaunga mkono wazazi au ndugu zao dhidi ya wake zao.
dah hapo kwenye red nimeipenda hyo mkuuUmenikumbusha film moja inaitwa Our Family wedding,baada ya wazazi na ndugu kuingilia sana mahusiano yao pamoja na harusi,mwisho wa siku jamaa akaweka msimamo na mtu wake kuwa "Their Wedding,Our Marriage" ukigundua hilo hawakupi tabu!
Mtambuzi,
Hapo kenye red pananipa tabu kidogo.
Ni potofu kwa vigezo vipi? Je vigezo hivyo ni universal? Nani anayesema/aliyesema potofu? Iliyonyooka inatakiwa kuwaje kuwaje?
Kama umeoa afu bado wazazi wana wa finance unategemea nini lazima wawe na sauti; he who pays the piper...
Kuna kijana namjua ni mtoto wa kiume pekee wa familia tajiri. Baba yake alifariki muda sana. Mama yake ana maela ya urithi kama hana akili nzuri. Huyo kijana amemuoa rafiki wa dada yangu. Wanaishi kwenye nyumba ya urithi; bonge la house kwa kuwa baba yake aliacha several houses tena zote ziko strategic areas.
Sasa mama mkwe wa huyo dada ana sauti mwanzo mwisho. Yani kuna moja ni kali jamaa alikuwa anatoka ulaya; mama kaenda kumpokea wakakutana na wife airport; mama akaamuru kijana aende moja kwa moja nyumbani kwake wameandaa dinner ataenda kwa mkewe kesho yake.
Haya mambo ya sijuho mtoto anapokea, sijuhi nini, mama anawaamulia mpaka wajukuu wavae nini.
Wamama kama hawa wanakuwa wamewalea watoto wao wa kiume kuwatii saana na huwezi kubadili hilo ni kukubali matokeo.
Na ukirogwa ukatamka sijuhi chagua moja mimi au mama yako, utazimia maanake possibility ya mama kuwa chaguo ni 99%
Watu kama hao wanaoa tu kutimiza wajibu but they feel that they have everything being with their family (mom and sisters)
Jibu lilikua baya lakini lilimsaidia sana badae yule muolewajihapo tu ndo patamu
Inakera sana vitu vya namna hiyo
thanks God hayo kwen baadhi ya ndoa hayapo.