Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kuna wanawake wakati wanaolewa waliwatukana wasioolewa na kuwaona wabaya na kuwachukulia wana mikosi
Kuna wanawake wakati wanaolewa waliwaona waliozalia nyumbani kama vile wana tabia mbaya wameshindikana na kuwadharau
Kuna wanawake wakati wanaolewa walijiona wazuri kuliko wasio olewa na hata kufikia kujiona wao ndiyo wazuri kwa kila kitu kuliko wasioolewa
Kuna wanawake wakati wanaolewa waliwaambia marafiki zao kuwa urafiki wao uishi ili wasije kuleta mazoea wakamuibia mume wake
Kuna wanawake wengine waliwafukuza ndugu zao wa kike kwa madai wanatembea na mume wake au wasije kutembea na mume wake. Wengine hawataki ndugu zao wa kike wawatembelee kabisa
Kuna wanawake wengine walikataa kusaidia kwao kwa madai yupo anapambana kujenga mji wake na wanae na mume wake.
Kuna wanawake wengine waliona ndoa ndiyi mafanikio yao ya mwisho,walipoolewa tu wakaanza maringo na dharau.
Sasa muda umepita na dunia ikawa mwalimu mzuri sana. Leo hii ndoa zimekua chungu kuachwa hawataki siyo kwamba wanapenda sana au wana heshimu sana ndoa zao bali hawana pa kwenda. Yaani hawana pa kwenda kwasababu wakati wanaolewa waliwatukana watu,kuwatenga na kuwaona hawawafai katika maisha yao.
Leo hawezi kurudi kwa dada zake sababu aliwatukana kuzalia nyumbani,hawezi kurudi kwa baba na mama aliwaambia hana hela anapambana na ndoa yake,hawezi kwenda kwa marafiki sababu aliwaambia wakae nae mbali wasije kumuibia mume wake.
Wamebaki kukubali kulala chini,chooni au jikoni au stoo ilimradi aonekane ana ndoa kuficha aibu ya matusi yake aliyotukana watu wakati anaolewa.
Wamebakia kutaka waachiwe nyumba ya mume wake kama mali ya kuachwa sababu akitoka hapo hana pa kwenda atakapoishi kwa amani.
Amebakia na unafiki wa ndoa,amebakia na majuto,amebakia na mawazo,amebakia kutapatapa,amebakia kujipendekeza kwa baadhi ya watu,amebakia kufanya visa na kutesa watoto akiamini anamkomoa mume wake.
Kama una binti, mtoto wa kike, dada narudia tena kama una binti,mtoto wa kike,dada tuwafundishe na kuwaambia ukweli kuhusu ndoa. Wasije kutukana watu sababu ya ndoa,wasije jitenga sababubu ya ndoa,wasije kunyanyasika na kuteseka sababu ya ndoa kwa kigezo cha kuvumilia.
Mungu siyo "asumani" kuweka talaka kwenye vitabu vyake VITAKATIFU.
Ndoa isikupeleke motoni kwa wewe unae amini.
Ndoa isikufanye ukagombanisha familia na koo za watu sababu ya kutoachana,ndoa isikufanye ukawa mnafiki au ukawa mchawi.