a woman can make or break her marriage....
Natumai wote mu wazima wanaJF.
Jamani kuna kitu chaniogopesha bado niko njia panda nahitaji kujua kwa kina.
Nakaribia kuingia kwenye ndoa,ninampenda huyu husband to be ila kila nisomapo,nionapo ndoa za ndugu jamaa na marafiki kwa kweli naogopa mnoo,nimechengachenga mara mbili ila safari hii sina ujanja.
Nachotaka kujua ni je maisha ya ndoa yakoje,mazuri,mabaya,kama uchumba au tofauti ni ipi na maisha ya boyfriend girlfriend?I wish kungekuwa na ndoa za mikataba hapa kwetu yani tumbo linauma kwa uoga. Je hii ni kawaida au nina tatizo la kisaikolojia?
Nahitaji michango yenu yenye busara.
Sweetdada.
Kwani Unaolewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki? Ndo utakuwa Mke wao?
Huna ujanja?Unataka ndoa ya mkataba?
Ukishaingia kwenye ndoa na mawazo ya aina hiyo tegemea sana kuhisi uko trapped utakapokuwa ndani.Kwahiyo jitahidi uondoe hizo fikra kichwani.
Kuhusu swali lako, pamoja na kwamba ndoa nyingi zinaonekana kuwa na matatizo usizitumie hizo.kama reference kwasababu tatizo halipo kwenye ndoa bali lipo kwa wanandoa.Wao ndio wenye matatizo. Hivyo wewe na mwenzako mkiingia kwa malengo, mkiwa tayari kusaidiana na kuongozana mtafurahia ndoa yenu. Jiandae tu kwa majukumu ambayo hukua nayo kipindi cha uchumba (kudeal na wakwe, mawifi na mashemeji, kuishi na mtu mwingine ambae anaweza akawa tofauti na wewe full time, kuwa msaada kwa mumeo n.k).
Alafu kama mlikua na uchumba mzuri na wote mlikua genuine mnaweza mkaendelea hivyo hivyo kwenye ndoa, plus majukumu zaidi. Kuweni marafiki, boresheni mawasiliano kila siku , heshimianeni maisha yatasonga.
Sasa sweeetdada hivi wewe unadhani ndoa zote zitakuwa sawa? Yani wewe na dada yako mlio zaliwa tumbo moja hamko sawa, vipi ndoa ziwe sawa.ni kijana mstaarabu na sio mvuta bangi, uoga wangu ni kutokana na ndoa nyingi nizionazo
ndoa unataka
na vya nje wataka...lol
Nadhani kuwa baada ya kuogopa sana, na kupiga chenga, na saa umefanya maamuzi ya kuolewa, umefanya tathmini ya mambo muhimu kwako.
nadhani umeshawaza jinsi utakavyojiepusha na mambo usiyoyapenda,
mengine unayaacha tu.
Muhimu kama walivyosema hapo juu usiingie ukiwa na lengo la kuvizia tatizo ukimbie.
matatizo yako mengi sana, hayana hesabu, mtazamo wako juu ya hayo matatizo, na reaction yako ndio itakayokutofautisha na hao unaowaona.
all the best, karibu kwenye chama kizuri ajabu, kama akili zako ziko kichwani