Jpinduzi
Senior Member
- Feb 26, 2011
- 136
- 68
Kila mtu atakubaliana nami kwamba ndoa ni sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu. Hili halina shaka ndani yake. Na wengine husema kwamba kama hujaoa au kuolewa, basi siku zote utahisi kuwa kuna kitu fulani katika maisha yako hujatimiza ili roho yako isawazike.
Ndoa asili yake ni tamu sana, ladha kamili ya maisha iko kwenye ndoa, ndoa ni kitulizo cha roho na nafsi,ndoa ni heshima kwa mwanadamu na ukamilifu wa Mwanadamu. Sina haja ya kuisifia ndoa saaaaaana maana kila mtu anatambua vyema thamani yake kama anavyotambua thamani ya jua. Lakini kinachoikwaza akili yangu siku zote ni ile patashika ambayo hutokea katika baadhi ya ndoa.
Katika Karne hii ya kizazi kipya cha Dot Com, utakuta asilimia kubwa mapenzi hupungua ndani ya Ndoa kuliko kabla ya ndoa. Utakuta wapendanao wanapenda sana kabla ya ndoa, wanaitana majina yote matamu duniani, Sweetheart, Honey, my love, darling, My heart, Baby, La azizi, mahabubu,....n.k.Lakini pindi wawili wapendanao -walio wengi- wanapoingia katika maisha ya Ndoa, basi Ndoa hugeuka na kuwa patashika nguo kuchanika, na si patashika tu bali pia hugeuka na kuwa pingu hasa pale wanapotakiwa kila mtu kutimiza majukumu yake yanayomlazimu kwa mwenzie.
Na hapo ndipo ndoa inapogeuka na kuwa ndoana, wanandoa walioitana majina yote matamu ya dunia hii kabla ya ndoa, wanafikia hatua ya kuchukiana kupita maelezo na kila mtu (kati ya wana ndoa hao) aliyejihisi alikuwa mfalme/malkia kabla ya ndoa sasa ndani ya ndoa amekuwa mtumwa wa taasis hiyo.Mambo yanapofikia hatua hii ambayo naweza kuiita mchafu koge, mapenzi ya wanandoa yanashuka kabisaaaa mpaka kufikia namba sifuri na mara nyingi grafu huenda chini ya hapo,na hapo ndipo utakaposikia wanaanza kuitana majina tofauti na yale ya awali. Utasikia "Mwendawazimu wewe, Shetani mkubwa, Ibilisi, *******, **** kama wewe unaweza kunioa/kuolewa na mtu kama mimi?
Hebu niangalie vizuri kwanza shape/elimu/utanashati wangu, unaona tuko sawa mimi na wewe au umekosea namba? Unaweza kuwa na mume/mke kama mimi, changudoa/serengeti boi wewe? Siwezi kutembea na wewe unanitia aibu barabarani, mwangalie sura yake, utadhani kalamba ndimu..." Basi wanandoa hao wote wanakunjiana sura, ukiwacheki utadhani konda kakosa abiria!.Ndoa inaendelea kuwa pilipili na hatimae wanandoa wanaamua kwenda hatua moja ya juu zaidi, kupigana masumbwi mazito mazito ya ki-Tyson na Evanda na kukabana ile kabari tunayoiita "Form six".
Hapo sasa ndipo swali linapokuja kwa wadau,ni kitu gani kinasababisha yale mapenzi ya kuhurumia, kupendana kuthaminiana, ikiwemo kuheshimiana kabla ya ndoa kugeuka ghafla na kuwa 'pingu' na hatimae watu kukabana kabari, kupigana vichwa, kurukiana sarakasi, kukabidhiana maumivu, kutoana ngeu, kung'oana meno, na mwisho kupeana 'karata 3'.??!!Hili ndilo swali langu,nawauliza ndugu zangu wadau, naomba mning'amulie na kunitegulia kitendawili hiki.Ni zipi sababu hasa zinazopelekea hali kuwa namna hiyo? SOURCE{ fotobaraza.me}