Ndoa ndoano!

Mh! Hapo pagumu,ila yeye ndio anafahamu kilichompelekea kufanya hayo aliyofanya. Aandike jina la yule ambaye yeye anampenda na yuko tayari kuishi nae. Afikirie vizuri kabla ya kufanya maamuzi isije baadae akatamani ku-undo.
 
hivi bado kuna watu hawavai kondom kwa vismall house na madebe yote ayo mnayopigiwa....khaa
 
kwa nini aliliambia hilo njemba la nje kuwa ana mimba yake wakati ana mume? angeongea kwanza na mume, akimtimua ndo aliambie hilo njemba.
 
Ajiandikishe makadi mawili. Kila baba na kadi lake.
 
Kama mume amekubali basi lakini itkuaje kw njemba?
 
Kwa mwanamke mvumilivu kuzaa nje eti kisa mume anakutesa na kulala nje sio suluhisho la tatizo. Haya sasa, mume kajirekebisha, yeye keshaharibu!
USILIPE UBAYA KWA UBAYA BALI LIPA UBAYA KWA WEMA!
 
Kitanda hakizai haramu, mtoto atakayezaliwa ni wa mume halali wa ndoa hilo halina mjadala.
 
Kama anataka aendelee kuwa na Mumewe..Kadi iwe na jina mumewe...... Kama amemchoka mumewe na anataka Divorce... Kadi iwe na jina la huyo jamaa....

Kama alivyoamua kutoka nje ya ndoa na kufanya mapenzi yasiyo salama basi kwa confidence hiyo hiyo afanye hayo maamuzi.....Sidhani kama kuna nafasi ya kusema nilifanya hivi kwa sababu fulani alifanya vile...Ni uamuzi wako..na ulikuwa sahihi wakati unaamua..iwe uamuzi mzuri au mbaya..
 

mwambie atumie baba cameroon easy
 
Wakutane wote watatu wakae chini wakubaliane kadi iandikwe jina la nani
 
ukipanda pilipili utavuna pilipili,sasa alienda ku do nje ya ndoa bila condoms tena tarehe za kushika mimba alitegemea nini,watu wengine bwana wanachefua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…