TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
UTANGULIZI.
Yamkini ndoa ni suala linalotambulika na takribani kila mtu dunia mzima,zipo ndoa kadhaa lakini mimi ninazungumzia ndoa ya mwanamke na mwanaume.
Sheria nyingi dunian ikiwepo ya Tanzania,na kamusi nyingi zimetafsiri kwamba Ndoa ni muunganiko wa HIARI kati ya mwanamke na mwanaume,ambao tayari wamekidhi vigezo vya kisheria kuanzisha mahusiano ,uchumba na hatimaye ndoa.
Kwa jamii nyingi ndoa ni ufahari hasa kwa upande wa mwanamke,wengi wanaamini ni heshima,ila kwa upande wangu najiuliza heshima kwa mwanamke kivipi? Yaani mwanaume ni wathamani sana mbele za mwanamke?,nitahitaji majibu.
Ili kufanya ndoa iwe timilifu kuna hatua na mambo kadhaa ambayo inabidi yafanyike kwayo mfano mwanaume au mwanamke (kwa baadhi ya nchi)kutoa posa,na mahali.
Utumwa ni ile hali ya mtu kutumikishwa katika mifumo mbali mbali,na hatimaye kutwezwa utu wake (Tafsiri yangu binafsi).
Posa ama kishika uchumba ni ni fedha ama kito chochote cha thamani ambacho mwanaume hupeleka kwa wazazi ama walezi wa mwanamke ili kutoa taarifa ya kutaka kuoana na binti yao,na kitendo hicho huitwa “kuchumbia”.
Mahali ni kitu cha thamani ambacho mwanaume analipa ili kutimiza takwa la ndoa,kamusi nyingi zimetafsiri Mahali kuwa ni kitu flani ambacho mwanaume hulipa kwa wazazi wa mwanamke anayetaka kuolewa kama shukurani kwa wazazi hao,shukurani hiyo inatafsiriwa kuwa ni ya malezi ba mengineyo ya muhimu,lakini huwa najiuliza kwani wazazi wa mwanaume hawakumlea mtoto wao? Mpaka wasipewe hiyo shukurani?.
NDOA NI UTUMWA WA MWANAMKE.
Mwanamke anafanywa bidhaa.
Mwanamke amegeuzwa kuwa bidhaa katika soko la ndoa ambapo mwanaume ni mnunuzi,kuanzia hatua za awali kabisa kuanzia kuchumbiwa.
Ili mwanaume achumbie anatakiwa kutoa Fedha,ama kitu chochote cha thamani,ili aoe inabidi alipe tena fedha ama kitu chochote cha thamani,sasa fedha hizo ama vitu hivyo ni sawa na kipimo cha thamani ya mwanamke,yaani mwanamke analinganishwa Thamani yake na Ng’ombe ama milioni kadhaa,kama si kutweza utu ni nini?,Sambamba na hilo katika kuitimiza azma hiyo ya kulipa mahali kuna nafasi ya kujitetea kwa mwanaume ili apunguziwe yaani kama unapoenda sokoni vile kununua nyanya,unaomba upunguziwe,sidhani kama nitakuwa nakosea kusema mwanamke analinganishwa na nyanya ama gunia la mkaa,kama si kuutweza utu wake nini?,na kibaya zaidi mwanamke akishasikia ndoa anawaka balaa kwa kuona ameula,nazani wanawake bado wapo gizani.
Hakuna mwanaume yeyote Yule ambaye ,leo hii tukisema mwanamke amlipie mwanaume mahali kama wanaume watakubaliana na hili,na ujiulize ni kwanini?
MAHALI NI CHANZO KIKUBWA CHA MANYANYASO NA UKATILI KWA MWANAMKE KATIKA NDOA.
Mwanaume kitendo chakumlipia mahali mwanamke basi anajiona ana hati miliki zidi ya mwanamke huyo,mwanamke atatambuliwa kuwa ni mfua nguo za mume,mpishi wa mume na mengine mengi,mwanamke atahesabiwa ni wachini kwa mumewe,kibaya zaidi vyombo vya dini na sheria zinakubaliana na hali na kitu chakushangaza zaidi ,wasomi washeria nao wameingia katika janga hilo nakuwafanya wake zao kuwa hivyo,na hata wanawake wenyewe wanakubaliana na hilo nab ado wanaenda mbali zaidi wakijinadi kama wamerogwa flani.
Asilimia kubwa ya wanaume wana vimba vifua kwa sababu tu wao ndio waliolipa mahali,(yaani mahali aliyolipa inampa kiburi zidi ya mwenzake),hii yote ni kwa sababu tu anaamini mahali imempatia hati miliki zidi ya mwanamke huyo,na ndio maana mwanamke asipopika mapema anacho,yaani ,asipofua anacho na makosa mengine yakishamba kabisa,ila mwanaume akitenda kosa mwanamke anyamaze aitwe mwenye heshima.
Huu ni ulimwengu ulioendelea,haki sheria,na usawa vinahesabiwa sana kwa masuala mengi lakini katika suala la ndoa sheria bado hazieleweki kabisa,na wasomi wa sheria wapo gizani na hii yote nadhani ni kwa sababu ndoa hufungwa kisheria lakini zinaishi kimila,desturi na utamaduni,yaani msomi kabisa anafanya mambo kwa sababu utamaduni wake unataka hivyo,na wala hajali kama sheria zinakataza kufanya tofauti.
KWANINI MWANAMKE ANALIPIWA MAHALI NASIO MWANAUME.
Nchi nyingi sana duniani ni mwanamke ndiye anayelipiwa mahali,baada ya hapo tunasema “KAOLEWA” na Mwanaume “KAOA”,ukiyatazama kwa undani maneno haya mawili(KAOA,KAOLEWA)yana ukakasi sana,na ndio maana ni ajabu kusikia mwanaume KAOLEWA,fikiri kwa kama mtu mwenye kichwa chenye ubongo wenye akili,haya maneno yanafanya upande flani uonekane ni wa chini na mwingine ni wajuu,niliwahi kusikia mwanaume akimwambia mwanamke “Kwani umenioa?” walipokuwa katika mgongano nilitafakari sana,kwa upande wangu mimi siamini kuna mtu anaoa ama anaolewa,bali naamini mwanamke na mwanaume “WANAOANA”na hakuna aliye juu wala chini ya mwenzake ila tamaduni za hovyo zinazolindwa na sheria za hovyo ndio zinaleta matabaka ya hovyo hovyo.
Zama hizo za kale kulitungwa,sheria maalumu iliitwa “KENTUTH”sheria hii iliamuru mwanaume kulipa mahali kwa mwanamwali ambaye hakuwahi kuingiliwa kimwili na mwanamume mpaka muda wa kuolewa kama shukurani ya kupata kitu safi kabisa,lakini kwanini iwe kwa mwanamke ,kwamba hakuna fahari yeyote kwa mwanamke kupata mume ambaye hajawahi kushiriki ngono kabla ya ndoa?,ama walimchukuliaje mwanamke?.
Baadae utamaduni huu uliendelea na kuzoeleka kwa wanawake wote,mpaka sasa,ili mwanaume na mwamke waoane ni lazima mwanaume atoe mahali ,na katika zoezi hili wazazi wa mwanaume ndio wanaopanga mahali ili binti yao achukuliwe,kibaya zaidi katika mfumo wa maelewano yaani biashara ni kupata,ukiondoa kwa dini ya kiislam.
Mimi nina amini kwamba na ndio uhalisia ,kwa mwanamke kulipiwa mahali ni suala la ubaguzi na unyanyasaji,maana huwezi kulinganisha thamani ya utu wa mtu kwa vito,kito kinachofanyika katika mfumo huo hiyo ni biashara,sasa tunapofanya mabadilishano ya pesa na mtu hiyo ni biashara ya utumwa.Huwezi kudai haki sawa wakati kunatamaduni na sheria ambazo kimantiki zinashusha hadhi ya mwanamke.
NINI KIFANYIKE.
Mapendekezo yangu,ili kuikomesha biashara hii ya utumwa ambayo imefichwa katika mwamvuli wa ndoa;
Mwanamke ni lazima aitambue thamani yake kwa kukataa yeye kulinganishwa utu wake na vito
Sheria za ndoa zitungwe kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa,na sio mila na desturi.
Kuoana liwe suala la hiari katika uhalisia wake na sio gelesha.
Wanawake waache kujiona ni watu wa chini(KUOLEWA) na wanaume ni wajuu (WAKUOA).nk
HITIMISHO.
Mimi kwa upande wangu natengeneza utamaduni wangu utakaoishi kwa familia yangu mimi tutaona na mwenzangu nitalipa mahali kwakuwa huu ni utamaduni ulioota mizizi,na watajijua wao,lakini hakuna mwananangu wa kike ambaye ataingia katika ndoa kwa mimi kupokea vito vya thamani ama fedha,yaani ni mlinganishe mwangu na fedha,haitawezekana(na nimeshaandaa usia kabisa ambao mwanangu mkubwa atasimamia hili endapo sitakuwepo hai)na mwanangu wa kiume mke atakaye oana naye kutoa ama kutotoa mahali ni suala la wazazi wa mwanamke,wakiona mtoto wao anathamani ya milioni tatu,poa tutalipa maana ndio akili yao itakavyo watuma
PINGA BIASHARA YA UTUMWA WA MWANAMKE.
Picha kwa hisani ya THE UNIVERSITY OF CHICAGO PRESS.

Upvote
1