Ndoa si ndoana ni kujaliana!

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Salam dadaz na kakazz...natumaini mlitumia weekend yenu responsibly na kuimaliza salama.Nawatakia jumatatu njema na wiki kwa ujumla!

Tuanze kwa kukumbushana jambo au mawili especially kwa wanandoa na wale wanaozisogelea!!!

Honestly nimechoka kusikia mtu anapotoa lalamishi kuhusiana na simu ya mke wake...watu wengi utasikia ohhh kwanini unampekua...simu yake we ya nini??Hapo hujawasikia wahusika wenyewe!!!

Seriously guys...ndoa si inaunganisha wawili kua wamoja???Sasa iweje kwenye ndoa kuwe na changu badala ya chetu??
Ushauri binafsi....kama mtu hauko tayari kuacha ubinafsi na mawazo ya changu changu subiri mpaka utakapokua comfortable na mawazo ya chetu.
Hayo mawazo ya simu yangu....kile na hiki changu ni ya kipindi cha upenzi...wakati bado hamjaamua kua kitu kimoja.

Hata mwili ukiwa ndoani sio wako tena!!Ni mali ya mwenzako as well....sasa unapoenda kutembeza mali ya mwenzio kwa mpango wa kando...kina dada poa....shamba boy na vidumu unajua kwamba hauna mamlaka hayo???

Embu ngoja nivute kaBible kangu ili tuelewane vizuri!!!
Wakorintho 7:4 inasema ''Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe.Hivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe.''
Hivyo basi....itunzeni miili yenu kwa niaba ya wenzi wenu kwasababu nyie ndo mnatembea nayo.Na muache ubinafsi kwenye ndoa.......hii inahusu hata swala la kunyimana unyumba!!!

Wakorintho 7:3 na 7:5 inasema hiviii ''Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.'' ila sio mu-overdo mpaka kulazimishana ikiwa mmoja hajisikii.....''Msinyimane isipokua mmepatana kwa muda, ili mpate faragha na kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokua na kiasi kwenu.''
Kwahiyo msinyimane wala msilazimashane!!Peaneni muda wa kupumzika ikiwa mmoja wenu anahitaji.....COMPROMISE...COMPOROMISE and MORE COMPROMISE itasaidia sana kupunguza nyumba ndogo and the likes!!

Nawakilisha!!!
 
Ulivyosema ni sawa.
Lakini uhalisia wa ndoa nyingi ni hiyo ya ndoa ndoana!
Wanandoa wengi wanaathirika kwa kuangalia sana filamu, video za kigeni na hata hizi za kibongo...zinazofundisha uchakachuaji wa ndoa... sio watu wengi wanazingatia mafundisho ya dini siku hizi..au maadili ya ndoa...kila kitu kinachakachuliwa.
Tunaiga iga kila kitu hata vile vibaya ,na tena familia zinakuwa kaa la moto.

Ni vizuri kukumbushana. tumefikia hali mbaya kuanzia mtu mmoja mmoja hadi taifa!
Ni hayo ya ubinafsi na changu changu tu.
 
Ndo maana tunakumbushana NONDA!Ni kweli nyingi ni ndoa ndoana ila si lazima iwe hivyo!Kama wawili wakijitoa kwa kila mmoja wao kweli kweli na kuridhika na wenzi wao matatizo mengi sana yatapungua!
 
Lizzy huu ushauri/reminder ni nzuri sana shida hapo kwenye kuiapply ndo utata.

BTW: Kukumbushana muhimu dear!!

DA
 
busara kubwa sana. hakika Mungu amekutumia na ubarikiwe kwa kukubali kutumika kusafisha njia ya injili ya Bwana. thank you and God bless you our today's greatest Evangelist, Lizzy
 
gud advice and reminder, kuutekeleza twahitaji kuongozwa na roho! barikiwa mpendwa
 
gud advice and reminder, kuutekeleza twahitaji kuongozwa na roho! barikiwa mpendwa

Asante mpendwa nawe ubarikiwe pia!Labda wawili watatu wataguswa wabadilike...
 
Pamoja na kuoana, lakini maisha binafsi kwa kiasi fulani hubaki palepale. Ni kama hii diagram hapa


Usidhani kuwa baada ya kuolewa kila kitu mtashea. Kumbukeni nyie ni watu tu mmekutana, na kuachana inawezekana, so private life should be respected.
 

Na hayo maisha binafsi yana-involve kufanya vitu ambavyo vitakua sumu kwenye ndoa yenu??I don't think so!!Sidhani kama kuna mtu anazunguka na mkewe/mumewe masaa 24 /7 kiasi cha kusema hana maisha tena asipokua na mwenzake kwasababu ata chooni hamfuatani.Usipompa mtu sababu za kutokukuamini wala hata simu yako hatahangaika nayo...ukiwa na marafiki zako hatakufuatilia!!
Mawazo ya kibinafsi kama yako ndo yanayosababisha ndoa nyingi ziwe na migogoro....kila kitu ni wewe...wewe...wewe tu....inakua kama hamna mtu mwingine kwenye picha!!
 

Salaam, ni ushauri mzuri Lizzy, however;
Katika uhalisia, nakubaliana na tuko katika mantiki ya ubinafsi usioadhiri set husika. Ubinafsi wa kuwa na wanawake au wanaume nje ya ndoa huo ni ubinafsi wa hali ya juu kabisa. ubinafsi wa kutaka kufanya maamuzi yanayo-affect set nzima bila subset nyingine kuhusika, hapo ni makosa makubwa.
Kuna mambo madogo sana ambayo si muhimu kwenye ndoa lakini yanalazimishwa kuingia kwenye set......kunyang'anya uhuru kwa degree zote wa mwenza wako.....

Haiwezi kutokea, just because mumeamua kuoana, basi muwe 100% compatible, Haiwezekani......sasa hapa ndo linakuja swala la COMPROMISE.....unataka sasa hivi, mimi sitaki sasa hivi.......tungojeane, au tutuvumiliane.

kila mtu lazima ana mambo bvinafsi amabayo angependa kufanya bila kuingiliwa, lakini hayaharibu SET (yale ya msingi katika ndoa)Kinachotakiwa ni mwenza kuyafahamu, asipoyafahamu utakuwa unakuwa mbinafsi, however, kama hujajua mambo binafsi ya mwenza wako katika kipindi cha microphone test one tw one two....basi hilo nalo ni tatizo.

Swala la simu naomba nisilisemee, coz ni janga la kitaifa sawa na kuwasikiliza mashoga/mashostito au wambea wa mtaani na kuamini kila neno.
 
Miongoni ya mambo ambayo yanasababisha ndoa nyingi kuwa ndoano ni kukosekana kwa uaminifu,hili ni janga la kitaifa.Uaminifu umepotea katika kila sekta,si biashara,serikalini na sasa katika familia.Kibaya zaidi watoto wetu wanachukua na kufanya kuwa sehemu ya maisha yao kwa kuwa wanaona yanatendeka.Sasa ukosefu wa uaminifu ukachanganya na ubinafsi unatamalaki hivi sasa ( Ingawa sijui kipi kilanza),hapo kila mtu anakuwa jicho kunyama mkono kumchuzi.Kukosekana kwa uaminifu,ubinafsi ukachnanganya na ukosefu wa uwajibikaji,hali inakuwa ya hatari zaidi.Kwa hiyo watu siku zote wamekaa kimitego mitego katika ndoa tukiamini wakati wowote tutagawana mbao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…