Mi nadhani alimaanisha kuwa ndoa ni zaidi ya upendo.
sio ndoa haiihitaji upendo, wala wanandoa hawatakiwi wawe na upendo.
lakini kwanza kabla ya kuenda mbali, je upendo maana yake nini?
kila mtu anaujua upendo kutokana na malezi yake, ndo maana hatuwezi kukubaliana na mwandishi huyo bila kujua upendo anaouzungumzia una maana gani.
mimi kwa mawazo yangu, upendo ambao ni msingi wa ndoa ni ule wa kuingia kwa hiari kwenya maisha ambayo una mtu pembeni yake ambaye umekubali akugande kwa siku zote, yani umakubali kuwa bosi wake, mfanyakazi wake, mama yake, baba yake, banker wake, mwanasheria wake, daktari wake, mzazi mwenzake, shareholder mwenzake, mhubiri wake muumini wake etc kwa siku zako zote zilizobakia.
mimi kwangu huu ndio upendo unaotakiwa, ila si hivyo tu kuna mambo mengine muhimu kama kutokujiachia sana huru kutaka kupata kila unachotaka.
mapenzi ambayo yakitangulizwa mbele ya ndoa lazima uvunjike ni hisia za matamanio ili ukiwa nampenzi unajisikia vizuri, unaona raha ukijisikia vibaya unavunja ndoa (ukishatanguliza hayo lazima utakuwa na ndoa moja kila mwaka)