Ndoa ya Jide kuvunjika, Gadner afunguka

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
HABARI kubwa ya mjini hivi sasa , hasa
kwenye mitandao ya kijamii ni juu ya madai
mazito ya kuvunjika kwa ndoa ya selebriti
wawili Bongo, staa wa muziki wa Kizazi
Kipya, Judith Wambura ‘ Lady Jaydee ’ au
‘ Jide ’ na mtangazaji maarufu wa Radio
Times FM , Gardner G . Habash , iliyofungwa
Mei 14, 2005, Ijumaa linamaliza utata .

KABLA

Kabla ya Gardner kufunguka , habari zilidai
kwamba wawili hao walikuwa kwenye gogoro
zito ambapo Gardner aliamua kuondoka
katika nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja
iliyopo Kimara - Temboni , Dar .
Ilidaiwa kwamba baada ya kuondoka
nyumbani eti Gardner alikwenda kukaa kwa
mmoja wa ndugu zake .
Habari hizo za kwenye mitandao ambazo
hazitaji chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ,
zilidai watu wa karibu na familia hiyo
walisema hiyo siyo mara ya kwanza kwa
wawili hao kutengana , lakini mzozo wa safari
hii unaweza ukawa wa moja kwa moja .

ACHA BWANA

Ilidaiwa kwamba ni kutokana na kutemana
huko, ndiyo maana Jide msanii anayetajwa
kuwa ni miongoni mwa wenye mafanikio
kimaisha Bongo, hakwenda Kituo cha Polisi
Oysterbay, Dar kumwangalia mumewe
ambaye aliwekwa korokoroni kufuatia kitendo
chao cha kuwakimbia askari wa usalama
barabarani akiwa na Ephraim Kibonde hivi
karibuni .

MAFUMBO?

Ilisemekana kuwa hisia za kuachana huko
zinachochewa pia na baadhi ya maandiko
ambayo mwanamuziki huyo wa Kibao cha
Yahaya , amekuwa akiyaweka katika akaunti
zake za mitandao katika siku za hivi
karibuni .
Ilielezwa kwamba katika akaunti yake ya
Mtandao wa Istagram, Jide aliweka picha
yake akiwa amesimama nje ya gari lake
kisha akasindikiza kwa kuandika hivi :
“Walking away from troubles”, maneno
ambayo kwa tafsiri isiyo rasmi yanamaanisha
kujiondoa kwenye matatizo .

BINTI MACHOZI?

Ilidaiwa kuwa kabla ya hapo , katika mitandao
inaandikwa kuwa Jide pia aliweka picha yake
akionekana kuwa na huzuni huku Binti
Machozi akilengwalengwa na machozi na
kusindikizia na maneno akiuliza : “Sijui
nisemaje ?”

GARDNER ANASEMAJE?

Mtu wa kwanza kupigiwa simu alikuwa ni
Gardner ambaye aliipokea na kabla
hajaelezwa chochote , alisema alikuwa katika
sehemu ambayo asingeweza kuzungumza ,
hivyo angempigia mwandishi wetu baada ya
robo saa.

JIDE VIPI?

Baada ya kukata simu, mwandishi wetu
alimwendea hewani Jide na baada ya kuita
kwa muda , simu yake ilipokelewa na Gardner
akasema: “Mpigie baada ya robo saa.”

DAKIKA 20 BAADAYE, GARDNER AFUNGUKA

Dakika ishirini baadaye , Gardner alimtumia
ujumbe mfupi wa simu mwandishi wetu na
kumweleza kuwa alikuwa Kituo cha Polisi
Oysterbay, Kinondoni jijini Dar ambako aliitwa
kwa ajili ya soo lao la kuwakimbia trafiki.
Baada ya kubadilishana maneno kadhaa,
baadaye aliamua kupiga na mazungumzo kati
yake na Ijumaa yalikuwa kama ifuatavyo ;
Ijumaa : Ebwana hivi hizi habari kwenye
mitandao juu ya kuvunjika kwa ndoa yako na
Jide zimekaaje ?
Gardner: Hamna kitu bwana, watu
wanaunganisha tu vitu sijui kwa sababu gani.
Ijumaa : Sasa kama ni hivyo kwa nini Jide
hakuja kukuona siku ile ulipolala polisi ?
Gadner : Unaona sasa , wao wanajua hivyo ,
lakini siyo kweli , Jide alikuja usiku sana kwa
sababu alikuwa anawaogopa mapaparazi .
Unajua Jide yeye huwa hapendi hayo mambo .
Alikuja usiku sana, lakini hata hivyo polisi
nao walimgombea sana kumpiga picha.
Ijumaa : Wanasema Jide kuna maneno
amepost kwenye akaunti zake mitandaoni
zinazoonyesha kuchoshwa na wewe ,
unasemaje?
Gardner: Si ndiyo kama hivyo nimekuambia ,
watu wanaungaunga tu vitu ambavyo
hawavijui na sisi hata hatujui malengo yao.
Wakati ule uliponipigia simu mara ya kwanza
nilikuwa naye kwenye gari ananipeleka pale
polisi , lakini akapaki mbali kwa sababu
hiyohiyo niliyokuambia kuogopa mapaparazi
na si unakumbuka hata ulipompigia kwenye
namba yake nilipokea mimi ?
Ijumaa : Kwani upo naye hapo sasa hivi
nimsalimie?
Gardner: Hapana tumeachana mimi niko
kwenye usafiri mwingine naelekea kazini na
yeye yupo kwenye misele mingine .
Ijumaa : Haya kaka basi poa .
Gardner: Poa kaka , mchana mwema .
 
Jide ni msiri sana na pengine alifanya hivyo ili waendelee kujiuliza na kuhisi.
 
Jide ni msiri sana na pengine alifanya hivyo ili waendelee kujiuliza na kuhisi.

Ana akili sana yule mwanamke, yani she lives on her own way, yupo makini sana na mambo yake yule, hana papara , anawachora tu wabongo wanavyojiropokesha mwenyewe kimyaa..
 
Ana akili sana yule mwanamke, yani she lives on her own way, yupo makini sana na mambo yake yule, hana papara , anawachora tu wabongo wanavyojiropokesha mwenyewe kimyaa..

Ahsante binamu kwa hii taarifa, nasubiri updates za majibu ya jide
 
Jamen udaku unakuja udaku unasepa hata siupati vizuri...
 
Kweli magazeti ukibaki kuamini vichwa vya habari bila kusoma kwa undani umekwisha.
 
Ana akili sana yule mwanamke, yani she lives on her own way, yupo makini sana na mambo yake yule, hana papara , anawachora tu wabongo wanavyojiropokesha mwenyewe kimyaa..

Kama yule bibi ambaye akikerwa kidogo tu na mwandani wake anakimbilia studio kurekodi unamwita ana akili sana, basi hakuna asiye na akili sana hapa duniani
 
Kama yule bibi ambaye akikerwa kidogo tu na mwandani wake anakimbilia studio kurekodi unamwita ana akili sana, basi hakuna asiye na akili sana hapa duniani

SANAA ni uwezo wa kuwasilisha mawazo yaliyo katika FIKRA za mwanadamu, Sometimes Wimbo ni njia mojawapo ya kuwasilisha mawazo/hisia za mwanamuziki, so sio vibaya kufanya hivyo as long as UJUMBE unasikika na kukubalika as long as hakuna wimbo wowote aliowahi kutaja au kumsema mtu unayemfikir wewe, ila kwa kuwa ni MJINGA na mvivu wa kufikiri ndio maana unafikiri NEGATIVE all the time kuhusu nyimbo za jide.
 
Samahani naomba kutoka nje ya mada kidogo....maana sijaingia humu kama wiki 1 hivi na kidogo, nimefarijika kumuona warumi humu kwa kweli, au ni Warumi mwingine? Pls niaminisheni kuwa ile kampeni ya #BringBackOurWarumi ilizaa matunda, ili niwape mucha thanks Mods kwa roho safi.
 
Last edited by a moderator:

Yani binam ukimpenda msanii atapambwajee!!
 
Yani binam ukimpenda msanii atapambwajee!!

Its Fact binamu, hata yeye alishasemaga kuwa nyimbo zake nyingi huongozwa na hisia na ndio maana akiimba anaimba kwa hisia na kufanikiwa kupeleka ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa

Nyimbo kama siku hazigandi, yahaya na machozi na nyingine nyingi alishawahi kukiri kuwa ni matukio ya kweli na kati ya vibao ambavyo vilifanya vizuri na kumpa tuzo kibao, so madai ya jamaa ni ya kishamba tu ina maana mtu asiimbe kile kilichopo moyoni? Huo ushamba na mawazo mgando labda kama ana agenda nyingine na jide.
 

Hihihiii Yes ni mimi binamu, nimerudi ila sio kwa ajili ya kampeni yenu ya #bring back warumi bali kifungo changu kiliisha so akina Invisible hawakuniachia kama mlivyotaka ila niliachiwa baada ya mda wangu kuisha, japokuwa ban yangu ilikuwa ndefu sana hata sijuagi kwa nini inakuwa ivi yani kila siku nikipata ban kifungo kinaongezeka.

Ingawa kampeni ya bring back warumi imesaidia tu kumfanya warumi arudi kwa kasi sana, so thanks sana kwa wadau wote akina Zalikina na wengine wengi tu, im back
 
Last edited by a moderator:

Team anaconda forever
 

Yote Heri binamu warumi ilimradi umerudi basi hakijaharibika kitu.
Ila jaribu kujicontrol unapokuwa una-argue na watu hasa wanaokuwa against wewe mkuu. Watupie kwenye ignore list tu ili kujiepusha na ban zisizo na lazma zinazoepukika, maana kuna thread moja hivi ya juzi niliona ulikuwa ushaanza kupanda temper na mdau mmoja. Jukwaa lilipwaya sana, now natambua uwepo wako mkuu.
 
Last edited by a moderator:

Shukrani sana binamu, nimekusoma sana
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…