Ndoa ya Kiba yamtoa povu Dully Sykes

Ndoa ya Kiba yamtoa povu Dully Sykes

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Dully-.jpg


Msanii wa muziki wa kizazi kipya , Dully Sykes, ametoa ya moyoni baada ya kutoalikwa harusi ya msanii mwenzake Alikiba, ambaye kwa asilimia kubwa amehusika kwenye sanaa yake ya muziki mpaka kufikia alipo sasa.
Akizungumza na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes amesema hajapewa taarifa yoyote kutoka kwa Ali Kiba licha ya kuwa mtu wake wa karibu, zaidi ya kuona mitandaoni na kuthibitishiwa na watu wa Mombasa.


“Mimi hajaniambia chochote na wala sijui, nimeona tu mitandaoni na nimepigiwa simu na dada yangu kutoka Mombasa, amenitaarifu kwamba Ali anaenda kuoa kule, lakini Ali hajaniambia chochote, mimi ni mtu ambaye nilikuwa namsapoti na ndiye nilianza kumkubali, kipindi hiko hakuna mtu yeyote anayemjua Ali Kiba, hata nyumba ya jirani hawamjui kama msanii, na niliposikia sauti yake tu nikamuomba collabo”, amefunguka Dully Sykes.


Hata hivyo Dully Sykes amesema anamtakia Alikiba maisha mema kwenye ndoa yake, kwani ni jambo la heri na kumsihi asichukulie mzaha suala la ndoa.

“Namtakia ndoa njema, nampenda sana na anajua, namtakia maisha mema, na namsihi ndoa sio kitu kidogo, anapoamua kuchukua mtoto wa watu, hasa ambaye amemchukua nchi nyingine, inabidi amuheshimu sana, amuonyeshe upendo hata yule mtoto akiitwa na wazazi wake mbona huji kutuangalia akose cha kuwaambia kwa upendo atakaompa”, amesema Dully


Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa Alikiba anatarajia kuoa hivi karibuni, ndoa ambayo imetangazwa kufanyika kwa siri nchini Kenya mjini Mombasa, na mpaka sasa mwanamke anayetarajia kuolewa na Alikiba hajajulikana ni nani kwa picha.



Chanzo: EATV
 
Dully amesahau kitu hapa. Kuna watu ni madaraja kwenye maisha ya watu. Umemsaidia kimuziki lakini jua ndoa ni kitu tofauti na muziki. Urafiki wako kwenye mziki sio wa kwenye ndoa.
 
Dully amesahau kitu hapa. Kuna watu ni madaraja kwenye maisha ya watu. Umemsaidia kimuziki lakini jua ndoa ni kitu tofauti na muziki. Urafiki wako kwenye mziki sio wa kwenye ndoa.


Hajasahau chochote, unamuonea tu. Kumbuka huyu ni mwanamme wa Dar na wanaume wa Dar wakisema kitu huwa hawafikiriagi, wanapenda sana kuropoka.
 
Sijaona Povu,kasema Ukweli Nani Asiyejua Mchango Wa Dully Kwa Watoto Wa Kariakoo Esp Gerezani
 
Collabo uombe wewe na kwenye harusi ulazimishe mwaliko. Pilau linawafanya watu wachanganyikiwe kabisa
 
Kumbe watu tunatofautiana sana haki, yaani mimi skuizi nisipo alikwa kwa harusi ndio kwanza nafurahia..... Maana masha yenyewe haya yamebana kuliko ugali wa kilasiku
 
Back
Top Bottom