Ndoa ya Lulu yabuma

Ndoa ya Lulu yabuma

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
BAADA ya kuwa na malengo ya kuolewa mwaka 2014 , mwigizaji Elizabeth Michael ' Lulu ' ameibuka na kusema imeshindikana lakini hajilaumu wala hamlaumu mtu yeyote kwa kutotimiza suala hilo kwani anaamini Mungu ndiye anayewezesha kila kitu.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni , Lulu alisema mwaka 2014 alikuwa na malengo mengi likiwemo suala la ndoa lakini kwa kuwa Mungu ndiye muweza, atapanga upya suala hilo na anaamini litakuja kutimia.

"Ndoa ni mipango ya Mungu , huwezi kulazimisha hata siku moja , sisi wanadamu huwa tuna mipango yetu lakini ili ifanikiwe lazima kuwe na baraka za Mungu , "alisema Lulu .

Akizidi kupiga stori na paparazi wetu , Lulu alisema kwa mwaka huu na mwakani hawezi kuweka malengo ya ndoa kwani bado kuna mambo yake hajayaweka sawa hivyo suala la kuolewa ataliweka hadharani baada ya miaka miwili ijayo .

"Sina mpango hata kidogo kwa mwaka huu wala mwakani labda baada ya hii miaka kupita ndiyo ninaweza kupanga tena suala la ndoa , " alisema Lulu .

Alipotakiwa kumtaja mpenzi aliyenaye kwa sasa , Lulu aligoma kufunguka lakini akakubali kuanika siri za mwanaume anayetaka kuwa mumewe .

"Kwanza nahitaji mwanaume atakayenielewa kwa kila kitu, pia awe na mapenzi ya kweli na atakayeniangalia kama Lulu na siyo kama Elizabeth pekee . Anapaswa kutambua na kusapoti kazi zangu za sanaa, " alisema Lulu .

Kuhusu mikakati yake ya sanaa mwaka huu, Lulu alisema ana mpango wa kuendelea na masomo huku akiwa pia na ' project ' kubwa mbili ambazo anatarajia kuzifanya.

"Nina project kubwa mbili mwaka huu, muda utakapofika kila mmoja atazijua maana nitaziweka wazi , " alisema Lulu .

Chanzo: GPL
 

Attachments

  • 1420440068513.jpg
    1420440068513.jpg
    41.3 KB · Views: 1,201
Kwa wanaume wa Bongo ahaaa Type hizo ndizo wanawakimbilia yaani ni kugombaniana ataolewa huyu soon ! Bakini na utulivu wenu hamuolewi mpaka muokoke muolewe na wenye Maja😛ound:nga!
 
Atakua kaachwa huyo,wakati anatangaza nia hakujua kuna Mungu?
 
Ndoa my a.ss
Umekuja na moto wa kiingeresa na wewe mwaka huu!!nakumbuka mlivosema ndoa ya uwanja wa taifa haitakuwepo jamaniii mpaka imeshindikana!kweli nyie kama vigagura wajamenii!!ha ha,natamani mseme CCm mwakani haiingii madarakani...
 
Umekuja na moto wa kiingeresa na wewe mwaka huu!!nakumbuka mlivosema ndoa ya uwanja wa taifa haitakuwepo jamaniii mpaka imeshindikana!kweli nyie kama vigagura wajamenii!!ha ha,natamani mseme CCm mwakani haiingii madarakani...

Hhhhhhaaaa mi na warumi tulikesha tunarogaa hakuna ndoaaaaa, na hiyo CCM inakaribia mwisho wakeee,,umenichekeshaaaa na siku ikifungwa tunahama jamii mi na@warumi
 
Last edited by a moderator:
Au ni lemutakozzzzzzzz ndo anataka kumuoa maana kuna siku alipost picha au ndo walikuwa kwenye mpango wa ndoa
 
Back
Top Bottom