Ndoa ya Sauda Mwilima ni shida

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Miaka miwili baada ya kufunga pingu za maisha ( ndoa ) na mwanaume aitwaye Kauli Juma , imefichuka kwamba ndoa ya prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima ina shida kwani haishi na mumewe, ikidaiwa kwamba kila mmoja anaishi nchi tofauti na mwenzake.

Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Sauda, kilisema kwamba baada ya wawili hao kufunga ndoa , Kauli aliondoka kwenda nchini Afrika Kusini ' Sauzi ' alikokuwa akifanya shughuli zake kabla ya kufunga ndoa na hadi leo hajawahi kurudi Tanzania .

"Yaani baada ya Sauda kufunga ndoa ,mumewe alikaa kwa miezi michache hapa Bongo, nasikia hata tendo la ndoa walifanya mara mbili tu .

"Hata alipojifungua na mtoto kufariki dunia kwa bahati mbaya , mumewe hakuwepo na hadi leo hajarudi, ukweli inauma sana ila Sauda ni mvumilivu kwani ndoa yake ni shida," kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo , mwanahabari wetu alimtafuta Sauda ambapo alikuwa na haya ya kusema : Sauda Mwilima akivishwa pete na mume wake, Kauli Juma . "Ni kweli anaishi Sauzi . Tangu tukiwa wachumba tulielewana kwamba tukioana kila mtu ataendelea kuishi anapoishi hivyo mume wangu anafanya shughuli zake nchini Afrika Kusini na huwa anakuja mara mojamoja akiwa na nafasi au akiwa likizo .

"Mimi siyo mtu wa kujionesha kwamba eti mume wangu yupo nchini hivyo akija huwa ni kimyakimya anakaa tunaendelea na mambo ya familia yetu basi muda ukiisha anaondoka na tulikubaliana tangu tukiwa wachumba hivyo ikitokea mmoja wetu ameamua kumfuata mwenzake na kwenda kuishi naye hakuna shida," alisema Sauda.

Sauda aliongeza kwamba ndoa yake iko vizuri na hawajaachana na endapo ingekuwa haipo asingevaa pete ya ndoa . "Ndoa yangu haijavunjika , tuko vizuri na mume wangu japokuwa tuko mbali lakini kila mmoja anamwamini mwenzake, " alisema Sauda.

Wadau wanaifananisha ndoa hiyo na ya Aunt Ezekiel na kudai kuwa wawili hao hawachekani.
 
huuu kweli umbea, eti walifanya tendo la ndoa mara mbili tu.,yaani akae miezi michache halafua afanye tendo la ndoa mara mbili tu inawezekanaje?
 
huuu kweli umbea, eti walifanya tendo la ndoa mara mbili tu.,yaani akae miezi michache halafua afanye tendo la ndoa mara mbili tu inawezekanaje?

Aahahahbahaha!! Mimi mwenyewe hiko kisehemu kimenigusa asieeh eti walifanya tendo la ndoa mara mbili dahh, warumi mbea lakini huyu katisha aiseeh, inabidi nimtafute, sasa sijui kajuaje kama walifanya ngono mara mbili tu kipindi chote cha uchumba hadi ndoa, dah mjini kutamu sana
 
Last edited by a moderator:
Mbona naona aliyeuleta hapa ni binamu yetu @ warumi
Eti binamu hiyo ya kufanya tendo la ndoa mara mbili tu ipoje hiyo?

Huu umbeya warumi kafunikwa.
 

Mpaka wewe mmbea uliyetukuka Afrika mashariki na kati umemnyooshea huyo mmbea mikono juu,kweli huyo mmbea kiboko.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hamsomi na kuelewa, source ni ijumaa wikienda.

Thanks, hao ni wafanyakazi wa shigongo mussa mateja na shakoor jongo, hawa ndo wambea wa gpl maarufu
 
Mbona naona aliyeuleta hapa ni binamu yetu @ warumi
Eti binamu hiyo ya kufanya tendo la ndoa mara mbili tu ipoje hiyo?

mmh mwenyew hawa akina mussa mateja wameniogopesha kwa kweli khaa, eti mara mbili tu walifanya ngono
 
Reactions: ram
Dah kweli kuna watu wamebobea kuzinyakua, eti wamefanya mara mbili tu
 
Habari za global zipigwe marufuku humu. Huo uchali wa ndoa yao uko wapi wakati wenyewe walikubaliana?

Mamaee zenuuu globo
 
Napenda mwanamke anaestiri ndoa yake,manake kwenye ndoa mashaka matupu.........
 
ahahahhhh,na yule dada yao sijui nani vile

mmh mwenyew hawa akina mussa mateja wameniogopesha kwa kweli khaa, eti mara mbili tu walifanya ngono
 
Halafu binamu hao hawafanyi ngono wanafanya tendo la ndoa, ni wanandoa hao, sio kama ndomo na mama ubaya

mmh mwenyew hawa akina mussa mateja wameniogopesha kwa kweli khaa, eti mara mbili tu walifanya ngono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…