Ndoa yampa presha Shilole

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

WAKATI akisubiri kufunga ndoa na mchumba wake, Uchebe Ashraf siku chache zijazo, staa wa muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ yu gonjwagonjwa, Ijumaa Wikienda limedokezwa.

Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao kilieleza kuwa, ndoa hiyo inampa presha Shilole kwani alizidiwa hivi karibuni na kwenda kulazwa hospitali licha ya kwamba kwa sasa anaendelea vizuri tofauti na awali.

“Unajua Shilole anatarajia kufunga ndoa na Uchebe hivi karibuni, kwa hiyo ana presha ya ndoa na ukizingatia na watu walivyozusha kuwa amerudiana na mpenzi wake wa zamani, Nuh Mziwanda ndiyo wakamchanganya kabisa,” kilidai chanzo hicho.

Ili kuujua ukweli wa habari hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shilole baada ya kuona picha alizosambaza mchumba wake Uchebe zikimuonesha mwanamama huyo akiwa amelazwa hospitalini ambapo alikiri kuzidiwa lakini akasema presha ya ndoa bali ni malaria.

“Jamani nililazwa hospitali kwa Dokta Mvungi kwa sababu nina malaria kali. Nilikuwa hoi, nikawekewa dripu, lakini kwa sasa ninaendelea vizuri na nimetoka hospitali,” alisema Shilole kwa sauti ya unyonge.


Muungwana
 
Kumbe ni habari za Ijumaa wikienda! Ngoja waje kina warumi
 
Ukiona ndoa ishaanza kukalowa vikao ujue haina mda mrefu
 
Huyo uchebe karidhika na zile Ndala?
 
Mi niliwahi kusema humu, Shilole ni wife material mkanicheka. Sasa maneno yangu yametimia.
 
Vijana wa mjini mna moyo sanaa kwa kuyavaa haya ma mama ya mjini.dahhh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…