ndugu nimekuwa kwenye ndoa kwa miaka 5 maisha yalikuwa mazuri sana. Tatizo limeanza mwaka mwanzoni pale nilipopata ugonjwa usio eleweka. Ghafla hali ilibadilika maumivu yakianzia kwenye unyao mpaka kiunoni misuli kuvuta ikiambatana na maumivu makali na UUME KUANZA KUINGIA NDANI YAANI KUWA MFUPI NA MGUMU NA MAUMIVU MAKALI YA MGONGO. NIMEPIMA MAGONJWA YOTE YA ZINAA SINA. X - RAY PAMOJA ULTRA SOUND PIA HAKUNA TATIZO. MITISHAMBA NIMETUMIA HAKUNA MABADILIKO NA NGUVU ZINAENDELEA KUPUNGUA MPAKA MKE WANGU AMETISHIA KUONDOKA KAMA MPAKA MWISHO WA MWAKA TAKUWA BADO SIJAPONA. NAOMBENI MSAADA WENU WA MAWAZO NA TIBA

jamani pole sana my dear! nimekuonea huruma wallah! sikiliza ushauri huko juu, MUNGU NI MWEMA ATAKUPONYA!
Nenda ukafanyiwe MAOMBI
Kwa Mungu Hakuna linsilowezekana, ila tu Vigezo na Masharti kuzingatiwa
kamanda pole sana mungu atakujaalia utapona..ila "kama hospital wanasema hawaoni tatizo" nenda kwa "wataalamu" wa tiba asili..waswahili walisema kikulacho mara nyingi huwa kiko nguoni mwako...kama upo dar panda basi nenda kibaha kwa mfipa kuna mtaalamu maeneo hayo naamini atakusaidia sana.
aisee magonjwa yapo mengi sana duniani...wanawake wachache sana katika 100 ni 1 tu ndio anaweza kuvumilia matatizo yanapotokea..ila cha msingi msihi asiondoke maana hujapenda kuugua na kama akilazimisha kuondoka let her go...wewe angalia matibabu ukipona wapo weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeengi sana
Hebu tujiulize je ni kweli dhana ya ndoa ni kufanya mapenzi? Jibu ni siyo kweli hata kidogo. Hebu tujiulize tena baada ya kuoana na kuishi kwenye ndoa kwa muda fulani wake au waume zetu wakapata matatizo ya kimaradhi au ajali au mengine ambayo yatawafanya wasiweze kabisa kushiriki jambo hili tutafanyaje? Huenda jibu kwa wale wanaoamini kwamba ndoa maana yake ni kufanya mapenzi watasema kwamba watakwenda nje au kwa wanaume wataoa wake wengine. Huu ni ujinga mkubwa mno kwani tunaweza kufanya hivyo ikiwa ni wenzetu waliopata matatizo lakini kama ni sisi tutaona inavyoumiza.
Tendo la ndoa katika ndoa ni muhimu na kwa kiasi cha kutosha husaidia pia kuimarisha uhusiano. Lakini pale kunapokuwa na tatizo kwenye suala hilo ndipo hapo upendo unapopimwa kama ni wa dhati, bandia, au upendo wa kimradi. Kama upendo wetu ni wa dhati tutajitahidi kuangalia mazingira ambayo huenda yatawafanya hao wenzetu wawe kama walivyo. Tunapojadili kwa upendo udhaifu fulani ni wazi tutawapa wengine nguvu ya kujikagua na kuzidisha upendo kwetu.
Lakini tunapokuwa wakali na kulaumu au kuchukia na kulaani tutawafanya wenzetu wajione wanyonge na pia tutawafanya au kuwapa nafasi ya kuhalalisha kwamba huenda sisi tumetawaliwa sana na tamaa ya kimwili kuliko uwezo wa kufikiri kiasi kwamba linapotokea tatizo tunakuwa vichaa na hivyo uwezekano wa kutoka nje au kuvuruga ndoa ni mkubwa. tujifunze kufahamu na kukubali ukweli kwamba ndoa bora na imara hazifanywi hivyo na tendo la ndoa, bali hufanywa hivyo na wanandoa kusaidia kutatua kila tatizo linalotokea.
Ni vizuri tukawa wazi kusema matatizo tunayohisi kwa wenzetu badala ya kuhisi tu na kudhani watayaona. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeshindwa jukumu letu la kupenda kwani tutakuwa tumejitazama wenyewe zaidi..