ndoa za siku hizi!!

kebi

Member
Joined
Jan 13, 2012
Posts
19
Reaction score
5
jamani maadili ya ndoa yameenda wapi kiapo cha kuishi pamoja kwa shida na raha mbona vyawashinda wanandoa. Tatizo nini hasa? Ndoa zavunjika kila kukicha kwanini?
 
..........unavyosema maadili ya ndoa una maanisha nini? Je kama ndoa haina maadili ya nini kuing'ang'ania?Hakunaga kuvumilia siku hizi, yakikushinda unasepa hukumbuki hata kama uliapa.
 
shida haiko kwa ndoa
ni wanandoa wa siku hizi
 
..........unavyosema maadili ya ndoa una maanisha nini? Je kama ndoa haina maadili ya nini kuing'ang'ania?Hakunaga kuvumilia siku hizi, yakikushinda unasepa hukumbuki hata kama uliapa.

Lol. .
 
Kuna mambo mengi sana yanayochangia ndoa nyini siku hizi kuto dumu, kwanza ni watu kutokuwa na hofu ya Mungu, unajua hofu ya Mungu ndani ya Moyo wako itakuzuia kufanya mambo mengi ambayo hayana maana.

Lakini pia jambo lingine ni tamaa, watu tumekuwa na tamaa ya kutaka kuishi maisha ambayo yako nje ya uwezo wetu, mtu huna uwezo wa kununua lakini unatamani kumiliki ndege, kwa hiyo watu wanaingia katika ndoa wakiwa na matazamio makubwa sana mwisho wa siku yanawashinda wanaanza ubabaishaji.

Kukosekana kwa uvumilivu, watu tumekwa si wavumilivu tena na kujifanya wajuaji jambo ambalo linaleta ushindani ndani ya ndoa na matokeo yake badala ya kusonga mbele mnaanza kushindana. Watu watumie muda kufahamiana vema kabla hawajaamua kuingia ndani ya ndoa, ndoa si mchezo wa kuigiza.

Mwisho kabisa ili niwaachie watu wengine nao nafasi ya kuchangia nadhani suala la watu kutokuonyesha uhalisia wa maisha yao toka mwanzo wa uhusiano nalo ni tatizo, be yourself kama unataka kufanikiwa katika mambo yako.

Mwombe Mungu akupe Mke mwema ama Mume mwema utaishi katika ndoa kwa amani na upendo.
 
Shida wattu wanaingia ili kukamilisha taratibu,kwamba nina mume,nina mke.. Hiyo yaani...

Ndiyo maana wanandoa wapya wa miaka hii kuanzia 2005 kuja sasa,si ajabu kila mwana ndoa ana mpenzi wake nje ya ndoa yake... Eidha wa zamani au mpya...
 
siku hizi wote watafutaji so ukinizingua nasepa mana i can take care of myself, na pia watu wengine wanaingia kwa matarajio fulani na wakiona akuna alichotarajia anasepa pia.
kulazimisha ndoa mana nilishawasikia wanaume kibao anaoa kisa msichana ana mimba wakiingia ndani mambo tofauti uzalendo unawashinda then kila mtu anafwata ustaarabu wake, akili kumkichwa.
 
Kazi kweli kweli. !!!!!!

The beautifull ones are not yet born.
 
tatizo ni wanandoa wanalazimisha ndoa au wanaingia kwenye mahusiano kwa masharti ya ndoa
 
inavunjika kutokana na wakati mnakutana hamkuvunji maagano mliyokuwa mumeweka na wapenzi wenu wa zamani ile kitu ni cha msingi sana hivyo unakuta msichana alikuwa na wachumba nyuma watano ,mwanaume alikuwa na wasichana saba na aliwaahidi ahadi mbalimbali ivyo cku wakikutana na msichana ambaye watadumu hadi wanaoana ,unakuta mchungaji anafunga ndoa ya watu 12 msichana 5+mwanaume7=12 iyo ndoa itadumu kweli wakati nafsi 12 zimefungwa kwenye ndoa moja?
 
jamani maadili ya ndoa yameenda wapi kiapo cha kuishi pamoja kwa shida na raha mbona vyawashinda wanandoa. Tatizo nini hasa? Ndoa zavunjika kila kukicha kwanini?

Umeoa au umeolewa? tupe kwanza sababu zako....
MM navyoona kuishi na mtu si ndugu yako kwataka moyo mvumilivu na upendo wa dhati...
 
mambo ya ndoa na viapo vyake ni full usanii tu siku hizi; watu hawachukui muda wa kutosha kutafakari haya mambo kabla ya kufanya committment badala yake wanarukia tu kwenye bandwagon kama fasheni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…